Miezi michache baada ya kipengele cha matangazo kuanzishwa, mtandao wa kijamii wa Instagram umekuja/unakuja vikali na kipengele chake cha matangazo hii yote ni ili kupata mapato zaidi kutoka katika mtandao huo.
Kutoka katika blog mtandao huo (Instagram) umesema kuwa utafanya mabadiliko makubwa katika upande wa matangazo. Moja kati ya mabadiliko hayp ni kwamba watangazaji wadogo wadogo na wakubwa wote wataweza kuweka matangazo yao kuanzia mwezi huu katika mtandao huo. Pia matangazo hayo yatapatikana kwa nchi zaidi ya 30 na itaachiwa kwa dunia nzima mwisho wa mwezi huu
Wazo hili limewajia instagram baada ya kuona watumiaji wa mtandao huo ni waaminifu baada ya kuachia kipengele hichi cha matangazo ( hawajapokea malalamiko baada ya instagram kuanzisha biashara yake ya matangazo). Baada ya muda tuu watumiaji wote zaidi ya milioni 300 wa mtandao wa instagram wataanza kuona matangazo kipindi wakiwa wanafanya yao katika mtandao huo.
Instagram pia watawezesha watangazaji kuenyesha video zenye sekunde 30 ambazo ni nyingi sana kwani sekunde za kawaida (zilizozoeleka mtandaoni humu) za kuonyesha video ni 15. Pia katika matangazo haya hata ule mfumo wa ‘landscape’ unaweza ukatumiaka vizuri tuu.
Katika matangazo hayo pia instagram itaboresha vipengele tofauti tofauti ili kuweka vibonywezo vya Shop Now, Sign Up, Install Now na Learn More chini ya picha. Baadhi ya makampuni yaliyojaribu kujitangaza kama vile Gilt Groupe na Made.Com yamesema kuwa yamejipatia faidi zaidi baada ya kujitangaza kupitia mtandao huo
Instagram pia wamesema wataendelea kuboresha vipengele hivi ili kupata matokeo mazuri kwa ajili ya watumiaji wake. Inaonekana macho mengi siku hizi ni kwenye pesa tuu sio? Haya watanzania na sisi tusubirie kuona matangazo haya. Ningependa kupata mawazo yako. Tuandikie sehemu ya comment. Tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKonaDotCom kila siku. TeknoKona Tupo Nawe Katika Teknolojia
No Comment! Be the first one.