Timu ya Instagram imezindua app leo ifahamikayo kwa jina la Hyperlapse. Hii ni mara ya pili kwa Instagram kutengeneza app nyingine tokea kampuni hiyo ilivyonunuliwa na Facebook mwaka 2012. Facebook walihakikisha Instagram inabakia kama kitengo kinachojitegemea kikiwa chini ya kampuni hiyo kubwa zaidi (Facebook).
App ya Hyperlapse inakuwezesha kurekodi hadi dakika 45 za video kisha kuongeza kasi ya video husika kwa kiwango cha hadi mara 12 ya kasi yake halisi. Hapa na maanisha kama unamrekodi mtu anayetembea basi kupitia app hiyo unaweza kuongeza kasi ya utembezi wa mtu huyu hadi mara 12 ya mwendo halisi aliokuwa anatembea. Kufanya hivyo kutaleta muonekano tofauti na wa kuvutia. Unaweza kuangalia video fupi kutoka kwao hapa;
Kiwango cha teknolojia cha kufanya hivyo kabla ilikuwa kunaitaji kamera za kisasa zaidi kama zile zinazotumika katika utengenezaji wa filamu za hali ya juu, hivyo timu ya Instagram kuweza kuingiza teknolojia hiyo kwenye app isiyokula nguvu nyingi ya simu ni jambo la kipekee sana. Inasemakana katika uhalisia utengenezaji wa video za namna hii kwenye kompyuta huwa zinatumia nguvu nyingi sana (RAM & Prosesa).

Kutumia App hii si lazima ufungue akaunti ila kwa watakaopenda wamepewa uwezo wa kuunganisha na akaunti zao za Instagram ili kuleta uraisi kutuma video kwenda Instagram moja kwa moja. Ila hata kama hutaunganisha bado unaweza kuchagua kama utapenda kuhifadhi video uliyokwisha itengeneza kwenye simu yako, pia unaweza kutuma kwenda kwenye apps zingine kama Facebook.
Kwa sasa Hyperlapse inapatikana kwa ajili ya watumiaji iOS (iPhone & iPad), bofya hapa kuipata, Instagram wamesema toleo kwa ajili ya Android litakuja baadae.
Tuambie kama umeipenda baada ya kuishusha kwenye simu yako? Kama unatumia Android endelea kuwa nasi tutakutaarifu pale App hiyo itakuwa inapatikana. Tufuate Facebook www.facebook.com/teknokona au Twitter @teknokona
Na hii ndiyo App yetu ya Wiki hii!
No Comment! Be the first one.