Instagram inaleta huduma ya 3D touch kwa watumiaji wa simu za Android, katika matoleo ya majaribio ya app hiyo maarufu unaweza kupata huduma ya 3D touch baada ya kubonyeza picha kwa muda mrefu kidogo.
Ingawa sio 3D touch kama ile ya kwenye toleo jipya la iPhone lakini hii ndio namna ya karibu zaidi kwa mtumiaji wa android kufurahia huduma hii ambayo ilitajwa sana wakati toleo la simu za iPhone lilipoingia sokoni.
Tofauti ya 3D hii ya Instagram na ile ya Apple
Ni ukweli kwamba 3D ya Apple ipo vizuri zaidi hasa ukizingatia kwamba wao wanauwanja mpana wa matumizi na sio kwa App moja tu, Instagram kwa upande mwingine ni kwamba hii 3D touch imedhibitiwa katika matumizi machache tu. Hata hivyo kama wewe ni mtumiaji mzuri wa Instagram basi hii itakurahisishia ku like kushare na kukomenti picha za marafiki zako.
Wakati 3D touch ya Apple wanatumia pressure sensor katika screen zao Instagram wanatuma screen za kawaida ila wanatumia muda wa mbonyezo.
kwa ufupi ni kwamba Instagram wanatumia njia tofauti kabisa na ile iliyotumiwa na Apple katika kufikia suluhisho moja la 3D touch, wakati Instagram wanatumia kubonyeza kitu kimoja kwa muda mrefu wao Apple wanatumia pressure sensor kupima mgandamizo iwapo unakua na pressure kubwa basi 3D touch hutokea.
Tutegemee nini baada ya hatua hii ya Instagram?
Ingawa Instagram hawajaanza kuitumia 3D touch rasmi lakini ni wazi kwamba watumiaji wa app hii watapata toleo jipya la kitumizi hiki hivi karibuni. Na kutegemea na mapokezi ya watumiaji wa app hii yatakuwa mazuri ( ambayo mpaka sasa ni mazuri) basi kuna uwezekano mkubwa sana watengenezaji wa app wengine pia wataiga hili na Android kwa ujumla itatawaliwa na app ambazo zinatumia aina hii ya 3D touch.
Je unailipataje toleo la Instagram ambalo lina 3D touch?
Kwa sasa toleo hili la instagram lipo katika majaribio bado na sio kila mtu anaweza kulipata kwa kupitia Playstore, lakini kama wewe unashauku ya kulipata toleo hili basi utalazimika kulipakua kwa njia ya faili la APK na ufuate maelezo haya ili kulishusha na kuinstall katika simu yako janja ya Android.
No Comment! Be the first one.