Haipingiki ya kuwa kamera za simu-janja zetu zinatumika kwa kupiga selfi siku hizi kuliko utumiaji mwingine wowote, na katika picha tunazopiga basi asilimia kubwa zinaishia Instagram. Na kutokana na utumiaji huu wa mtu mmoja mmoja basi tumeweza isaidia Instagram kukuwa kwa kasi zaidi katika miezi tisa iliyopita kufikia kiasi cha kuufunika mtandao mwingine maarufu wa Twitter kwenye wastani wa watumiaji kwa mwezi.
Hivi sasa Instagram imefikisha wastani wa watumiaji milioni 300 kila mwezi na hivyo kuiweka mbele ya Twitter ambayo imeripoti kuwa na wastani wa watumiaji milioni 284 kila mwezi.
Takribani picha milioni 70 zinawekwa kwenye mtandao wa Instagram kila siku!
Kundi kubwa zaidi la watumiaji wa Instagram wanatoka katika umri wa miaka 18 hadi 24 na wengi wao wapo nje ya Marekani.
Instagram ilinunuliwa mwaka 2012 kwa dola bilioni 2 za Marekani na kampuni ya Facebook, na ununuzi huu umewasaidia sana katika kusaidia ukuaji huu wa Instagram.
Instagram ina miaka minne tuu, ikilinganishwa na mitandao mingine data zipo hivi
- Facebook iliyopo kwa miaka 10 sasa ina wastani ya watumiaji bilioni 1.35 kwa mwenzi,
- YouTube iliyopo kwa miaka 8 sasa ina wastani ya watumiaji bilioni 1 kwa mwezi,
- Twitter ina miaka nane na ina wastani ya watumiaji milioni 284!
Kumbuka kuungana nasi kwenye mitandao mingine (bofya); Facebook Twitter na Instagram
No Comment! Be the first one.