Miezi miwili iliyopita mtandao wako wa Teknokona ulikuletea habari kwamba Instagram walikuwa wanafanya majaribio ya watumiaji kuwa na akaunti zaidi ya moja katika app zao za iOS na Android. Wameleta uwezo huo sasa!
Baada ya majaribio na marekebisho hatimaye Instagram wameachia toleo jipya la Instagram ambalo lina mruhusu mtumiaji kuweza kumiliki akaunti zaidi ya moja.Toleo hili jipya la Instagram ambalo ni toleo la 7.15 limeanza kupatikana kwa baadhi ya watumiji wa Android na wale wa iOS na baada ya muda litakuwa linapatikana kwa watumiaji wote.
Hatua za kufuata ukishasasisha(update) app yako
Nenda katika ukurasa wa akaunti yako kisha ubonye sehemu ya mipangilio (settings) ambayo ni kulia juu kama ilivyooneshwa katika picha hapo chini.
Shuka chini mpaka utakapo onasehem ya kuongeza akaunti nyingine (add account) kama inavyoonekana katika picha hapo chini.
Ingiza taarifa za akaunti yako ya pili na kisha ingia (log in)
Hizi ni taarifa nzuli kwa mablogger na watu wote ambao wanamiliki ama kuhudumia akaunti zaidi ya moja katika mtandao huu wa Instagram, mfano kwangu mimi kuanzia leo ninaweza kuihudumia akaunti yetu ya Instagram ya TEKNOKONA na huku nikiendelea kupatikana katika akaunti yangu binafsi ya Instagram
Instagram wanatofautisha akaunti hizi mbili kwa kutumia rangi za background, kwa upande wa notification utapata notification kutoka katika akaunti zote ulizonazo katika app yako ila kama unataka akaunti moja isilete notification basi utatakiwa kuzima katika mpangilio wa akaunti hiyo.
Bora kuchelewa kuliko kukosa kabisa, hii ni moja ya huduma ambayo watumiaji wengi wa instagram walikuwa wanaitamani na sasa imefika.
Huduma hii kwa kwetu Afrika Mashariki inakuja na mazuri pamoa na mabaya, mazuri ni kwamba watu ambao wanamiliki ama wanahudumia akaunti zaidi ya moja watapata nafasi ya kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.
Kwa baadhi ya watu huduma hii ya akaunti zaidi ya moja katika app itakuwa ni nafasi kwao ya kufanya uhalifu wa kimtandao kwa kufungua akaunti wakijifanya watu fulani (parodies) na pengine hii itaongeza utaratibu wa matusi katika mtandao huu wa Instagram.
No Comment! Be the first one.