Kila kitu kizuri kina ushindani na katika suala zima la teknolojia ambayo ina vitu vipya mathalani mtandao wa kijamii, Instagram umezidi kupanua wigo wake wa biashara siku hadi siku.
Mwaka 2018, Instagram imeamua kujiweka sawa kabisa na kupambana na Youtube kwani kitu ambacho wamekizindua kinaweza kuleta upinzani sana hasa kwa wale wanaotumia Instagram sana.
Instagram wamezindua IGTV lakini je, unafahamu ni nini?
IGTV ni kipengele na lakini vilevile ni programu tumishi mpya inayojitegemea ambayo inamuwezesha mtu kuweka video (picha jongefu) yenye urefu usiozidi dakika 60 yaani saa moja. Kama wewe ni mtu unayetumia Instagram utakuwa unafahamu hapo awali mtu aliweza kuweka Instagram video isisyozidi dakika moja.
Vilevile, kipengele cha IGTV kimewekwa pia kwenye tovuti ya instagram hivyo hata bila kutumia programu tumishi ya Instagram/IGTV yenyewe bado utaweza kuweka video yenye urefu wa saa nzima au chini ya hapo kupitia tovuti yao.
Kitufe cha IGTV kwenye programu tumishi ya Instagram.
Je, IGTV ipo kwa wote (Android/iOS)?
Jibu ni ndio IGTV inapatikana kwa wenye simu rununu zinazotumia mfumo endeshi wa Android/iOS lakini kipengele hiki kinaangazia zaidi zile akaunti za muda mrefu/zenye watu wengi wanaowafuata hivyo basi kwa akaunti mpya za Instagram au wenye watu wachache wanaona machapisho yao (followers) hawataona kipengele cha IGTV kwenye vifaa vyao.
Hakuna matangazo kwenye IGTV kwa sasa lakini kwa siku za mbeleni matangazo yatakuwepo kwani Instagram wanaamini kuwa huko ni sehemu nzuri ya kuweka matangazo.
IGTV inaweza ikawaongezea Instagram mara dufu kwani watu wengi wamekuwa wakiomba kurefushwa kwa muda wa video ambao mtu anaweza akaiweka huko.
Wengi wanaamini kuwa IGTV italeta upinzani mkali kwa Youtube baada ya kupiga hatua kubwa kwa kuongeza dakika hamsini na tisa kwa kila video ambayo mtu ataiweka Instagram. Mambo ya kwenda mubashara sasa yataongezeka!
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|
One Comment
Comments are closed.