Intel ni moja kati ya kampuni kubwa sana ulimwenguni katika maswala ya teknolojia vivyo hivyo kampuni ya Asus ambayo inasifika sana kwa vifaa vyake vya kiteknolojia kama vile kompyuta n.k
Kampuni hizo mbili (Asus na Intel) wameona waingie katika ushirikiano ambao utawawezesha wawili hao kuja na ubunifu ambao utapelekea kuzalishwa kwa kompyuta ndogo/yenye umbo dogo.
Makubaliano haya yanahusisha moja kwa moja kutengeneza, kuuza na kutoa msaada wa kitaalam kwa bidhaa zinazojulikana kama NUC (Next Unit Of Computing) na haswa katika kompyuta zenye umbo dogo.
Kwa haraka haraka ni kwamba kinachofanyika hapa, makampuni yote mawili yapo katika makubaliano ili kuhakikisha kwamba bidhaa za NUC zinasonga mbele.
Katika utengenezaji na uuza wa kompyuta zenye umbo dogo, Asus na wao hawabaki nyuma kwa mfano wana yale matoleo ya kompyuta zao za Chromebook zenye umbo dogo.
Intel wao mwanzoni mwa mwezi huu waliweka wazi kwamba wao kama wao hawataki kufanya uwekezaji wa moja kwa moja katika bidhaa zao za NUC lakini kama akitokea mshirika mwingine wataingia nae katika makubaliano.
NUC ni moja ya kompyuta ambazo zina umbo dogo kabisa –pengine unaweza hata kuzishika kwa mkono mmoja—lakini zinafanya kazi kama kompyuta zingine tuu.
Kupitia makubaliano haya ni kwamba Asus wataanza kutengeneza kompyuta na kuziuza kupitia NUC ya Intel kwa kibali maalum,
Vile vile Asus watakua watafungua tawi lingine kwa ajili ya biashara hiyo linalojulikana kama “ASUS NUC BU” ambapo kazi kubwa itakua ni kutoa msaada wa kitaalam kwa ajili ya wateja wa NUC.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je hii umeipokeaje? Kwa haraka haraka unaona makubaliano haya yana tija?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.