Kivinjari cha internet explorer ndio cha kwanza kwa umaarufu katika vivinjari vyote, umaarufu huu ulikifanya kuwa namba moja kwa muda.
Kumbuka hapo awali Microsoft ilikitupa kivinjari hicho cha Internet Explorer katika Windows 11 na kubakia na Micrsoft Edge, ambacho ni kivinjari shindani kabisa na Chrome, Safari, Mozila na vingine vingi tuu.
Hizi ni moja kati ya jitihada za kufanya kivinjari cha Edge kuzidi kupata watumaiji wengi Zaidi na kuzidi kukuwa. ukaichana na hayo yote hata hivyo kivinjari cha edge kina uwezo mkubwa kulinganisha na hiki.
Ufanisi, uimara na ufanyaji kazi kwa ujumla bado uko kwa upande wa Edge kama hivyo viwili vikilinganishwa lakini hata hivyo kwa watumiaji wa matoleo ya nyuma kwa Windows 10 kivinjari hicho hakitafutwa bali kitakuwepo kama kawaida.
Hapo awali tuliandika kuhusu windows 11 kuifuta internet explorer kabisa soma >>HAPA<< kuhusu Makala hiyo.
Kingine cha kujua hapa ni kwamba kivinjari hiki sio kama kitafutwa, kitakua kinaonekana kama kawaida katika maeneo yote (kinapoonekanaga)
Lakini kinachobadilika ni kwamba ukikifungua kitakua kinafunguka kivinajari cha Edge (Microsoft Edge). Mabadiliko haya yataanza kutekelezwa rasmi juni 15, 2022
Ningependa kusikia kutoka kwako,niandikie hapo chini katika eneo la comment, Je unadhani ni sawa kwa kampuni kuachana na kivinjari hicho?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.