Kutumia toleo la karibuni kabisa linalohusisha programu endeshi au masasisho mengine yanayotolewa kwa maana ya kukifanya kifaa kiwe salama zaidi si jambo la kupuuzia hata kidogo na hii ni wa watumiaji wa Android halikadhalika iOS.
Ni miaka karibu miaka kumi na minne sasa tangu iPhone ya kwanza itoke huku ikiwa na mfumo endeshi wa iOS 1 na sasa imefikia toleo la 14 na kuzidi kupata wateja wengi zaidi kila baada ya kipindi fulani. Unafahamu sifa za iOS 14? Soma zaidi kwa KUBOFYA HAPA.
Kwa watumiaji wa iPhone kuanzia toleo la 6s mpaka iPhone SE 2020 wanaweza kushusha toleo hilo, iPhone 12 na familia yake nzima zenyewe zinakuja zikiwa na iOS 14 tayari.
Kwa mujibu wa takwimu za karibu kabisa kutoka kwa Mixpanel zinaonyesha kuwa mpaka sasa 90.45% wanatumia iOS 14. Mwezi Februari, Apple ilisema iOS 14 ilishafika 86% kwa vifaa vyote vilivyotoka ndani ya miaka minne iliyopita, 80% ya iPhone zinatumia iOS 14.

Kwa haraka haraka tuu takwimu za karibu zinaonyesha ni 11% pekee ndio wanatumia Android 11 nchini Marekani? Je, wewe iPhone yako inatumia toleo la karibuni kabisa? Namaanisha iOS 14.5.
TeknoKona tumekuhabarisha hivyo basi usiache kutufuatilia kila inapoitwa leo.
Vyanzo: 9to5Mac, GSMArena
No Comment! Be the first one.