Watumiaji wa bidhaa za kampuni ya Apple sasa wanaweza kufanya maboresho ya program za uendeshaji wa bidhaa kama iPhone, iPad na iPod Touch.
Ina maboresho mbaimbai ingawa bado wadau wengine wanadai si mengi sana na Apple wangeweza fanya zaidi. iOS 6 imetoka kwa ajili ya simu za iPhone 3GS, iPhone 4, iPhone 4S pamoja na iPhone mpya ya iPhone 5. Pia inafaa kwa iPod Touch 4 na 5, kwa upande wa iPad ni iPad 2 na iPad 3.
Vitu vipya katika toleo hili ni pamoja na huduma za Facebook kuboreshwa katika matumizi mbalimbali, mfano ukishapiga picha unaweza kutuma Facebook hapo hapo bila kuhamia kwenye program ya Facebook. Hivyo utaweza ku’share’ vitu kwa urahisi zaidi kwenda Facebook, ingawa hii ni mara ya kwanza kwa iOS kitu hiki kipo muda mrefu kwenye tablets na simu zinazotumia Android.
Upande mwiingine ni program ya matendo kutokana na sauti, inayofahamika kama Siri. Kupitia Siri utaweza fanya mambo mengi kwa kuongea na simu, tablet au ipod yako. Lakini sio Kiswahili, (hahahahah 🙂 ) Kwa sasa lugha zinazotambuliwa na programu hii ni Kiingereza, Kifaransa, Kichina, Kikorea, Kijapani, Kijerumani, na Kiitaliano, hivyo kama upo safi katika hizi lugha basi hata kama ni kuandika ujumbe mfupi wa maneno (sms) wewe utaongea tuu nayo itajiandika.
Mabadiliko mengine makubwa yanayolalamikiwa ni pamoja na kampuni ya Apple kuondoa huduma za ramani kutoka kampuni ya Google, Google Maps, na kubadilisha kwa kuleta huduma za ramani kutoka Apple. Kampuni ya Google inauzoefu wa muda mrefu katika hili hivyo bado Apple hawajafikia kiwango cha juu cha huduma hizi kama Google, lakini kutokana na ushindani wao unaokua inaaminika ni moja ya sababu ya uamuzi huu. Si hapo tu, bali hata programu ya huduma za YouTube kutoka Google ambayo tokea iPhone ya kwanza hapo mwaka 2007 ilikuwa inawekwa pamoja katika programu ya uendeshaji, kwa sasa imetolewa, hivyo kama bado unapenda kuangalia video mbalimbali kutoka YouTube basi itabidi uipakue (install) mwenyewe kutoka soko la programu (App Store).
Mambo mengine ni maboresho tuu ya huduma mbalimbali kama za FaceTime (huduma kama Skype kwa watumiaji wa iPhone, iPod Touch na iPad, pia kuna maboresho katika huduma za barua pepe. Kwa sasa barua pepe zinapewa sura ya kitofauti. Pia kwa sasa utaweza kuweka (attach) picha na video wakati unaandika barua pepe, hichi ni kitu cha kawaida kwa watumiaji wa bidhaa zinazotumia Android lakini kwa za Apple ndo kwa mara ya kwanza hichi kitu kinawezekana.
Kwa sasa unaweza kupata iOS 6 kwa bidhaa nilizozitaja hapo juu kwa njia zifuatazo, kwa kutumia laptop/kompyuta yako hakikisha una iTunes (12.7) ya kisasa zaidi, kama huna nenda hapa http://www.apple.com/itunes/download/ , ukishaipakua kwenye kompyuta yako unganisha iphone, ipod touch au ipad kisha fungua iTunes.Unganisha kifaa chako basi ujumbe utakuja kukuambia kuna toleo jipya la ‘firmware ios6’, bofya ‘Download and Install’, iTune itashusha na kupakia programu ya iOS 6 kwenye kifaa chako.
Mfano: Bofya ‘Update’ |
iOS 6 ni faili kubwa, takribani 1.1GB, hivyo kama unawasiwasi na njia hii unaweza kulishusha moja kwa moja kupitia ‘links’ zifuatazo.
Download iOS 6 for iPhone:
Download iOS 6 for iPad:
iOS 6.0 (iPad 2 Wi-Fi): Link
iOS 6.0 (iPad 2 GSM): Link
iOS 6.0 (iPad 2 CDMA): Link
iOS 6.0 (iPad 2 New): Link
iOS 6.0 (iPad 3 Wi-Fi): Link
iOS 6.0 (iPad 3 GSM): Link
iOS 6.0 (iPad 2 GSM): Link
iOS 6.0 (iPad 2 CDMA): Link
iOS 6.0 (iPad 2 New): Link
iOS 6.0 (iPad 3 Wi-Fi): Link
iOS 6.0 (iPad 3 GSM): Link
Download iOS 6 for iPod Touch:
iOS 6.0 (4G): Link
Baada ya kulishusha (download) unganisha kifaa chako na kompyuta, nenda iTunes, upande wa kushoto wa iTunes, Devices, chagua kifaa chako. Bonyeza kwenye Keyboard ‘Shift’, bila kuachia ‘Shift), bofya (click) ‘Restore’ kwenye iTunes. Chagua faili la iOS 6 ISPW uliloshusha kutoka mtandaoni, achia iTunes ifanye kazi yake.
Njia nyingine ni kupitia hiyo simu, ipod au ipad yako, nenda kwenye Settings, afu General, bofya kwenye Software Update, shusha iOS 6.
Kwa wale tunaotumia zilizokuwa ‘JailBroken’ basi itakubidi usubiri hadi pale hackers watakapotoa ‘JailBroken iOS 6 firmware’, kwani vinginevyo kuna uwezekano mkubwa utapoteza data zote ukiingiza ios6.
Muhimu; Kumbuka kufanya ‘Back up’ ya kifaa chako kwenye iTunes kabla ya kufanya mabadiliko haya.
No Comment! Be the first one.