Jinsi wateja wanavyozidi kufurahia iPhone 6 na 6 Plus bado wana shauku ya kujua nini kipya kitatoka tena hasahasa kwenye iPad. Ripoti kutoka Apple Inc ni kwamba wateja wake wategemee iPad Air zenye rangi ya dhahabu (Gold) pia kuingia sokoni, na hii ni sababu wanataka linganisha na rangi za iPhone ili kuleta uwiano kidogo.
Pia kuna fununu kuwa iPad mpya zitakua na sensa za vidole (Touch ID fingerprint sensor) kama kwenye baadhi ya simu za iPhone. Apple pia wanatarajia kuleta ‘Mac OS X ‘ update (version 10.10 Yosemite) pamoja na iPod mpya sokoni . Japokua soko la ‘Tablets” limeshuka kwa ujumla lakini bado wapenzi wa bidhaa za Apple wanasubiria kwa hamu matoleo mapya ya bidhaa zao zijazo. iPad hii inatarajiwa kuwa na kioo kikubwa chenye ukubwa wa ‘Inchi 12.9‘
Kwa kawaida kampuni huwa inaachia matoleo mawili, toleo la mwezi Septemba ambapo wanatoa toleo jipya la iPhone na toleo la mwezi oktoba amabapo wanatoa iPad mpya . Kwa mfano mwaka jana mwezi oktoba Apple Inc walitoa iPad Air, iPad Mini yenye ‘Retina Display’ na kuachia ‘OS X Mavericks’.
Hivyo mwisho wa mwezi huu tutegemee vitu vifuatavyo; iPad Air 2, iPad Mini, kompyuta mpakato (laptop) mpya za toleo la MacBook pamoja na mboresho (update) mpya kwa toleo la programu uendeshaji ya OS X Yosemite.
Je, unahisi kwa toleo hili la iPad ya rangi ya dhahabu litakamata soko la Tableti?
Kusoma kuhusu iPhone 6 na iPhone 6 Plus BOFYA HAPA!
No Comment! Be the first one.