Kwa siku mbili mfululizo zimezuka habari kuwa kampuni ya Apple watengenezaji wa simu za IPhone, pamoja na tablet maarufu za IPad, wanaweza kuwa katika utengenezaji wa IPad ndogo katika ukubwa, na zitakazokuwa bei ya chini zaidi ili kuweza kushindana na tableti za ukubwa huo za android kama Kindle Fire na Nexus 7 kutoka Google.

Kampuni ya Apple bado hawajatoa taarifa ya kuthibitisha habari hizi, ila hadi sasa vyanzo vingi vya habari katika tovuti mbalimbali kama Mashable, PCWorld na wengine wanaamini IPad Mini inaweza ikawa sokoni kabla ya mwaka huu ujaisha, hasa hasa ndani ya kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka.
![]() |
Kampuni Ya Google Imeingiza Tablet Ya Nexus 7
|
Wengi wanaamini kwa kutoa IPad Mini kampuni ya Apple watazidi kulishika soko la tableti dhidi ya Kindle Fire, Nexus 7, Galaxy Tab na wengine. Kwani tableti ndogo itaweza kunuliwa na masoko mengi duniani hasa yale ya nchi zinazoendelea ikiwa pamoja na Uchina. Kweli tableti ya nchi 10 ni ghari sana (utaitaji zaidi ya laki 5 na nusu kupata IPad mpya kwa sasa), ila kwa IPad Mini inaaminika itauzwa takribani Tsh 370,000/=.
Kuongezeka kwa utumiaji wa vitabu vya digitali (e-books), intaneti n.k inaaminika soko la tableti litazidi kukua hasa kwenye nchi zinazoendelea.
Lakini pia wapo wanaoamini uhamuzi huu hautakuwa mzuri kwa kampuni hiyo, kwani itawafanya watu wengi waliokuwa na madhumuni ya kununua IPad kubwa kuchagua ndogo hivyo kampuni hiyo kuwa inajiharibia soko lake linyewe. Kwa upande wangu nadhani huu utakuwa uamuzi mzuri na utakaoisaidia kampuni hii katika ushindani wake na tableti zinazotumia Android ambazo zinazidi kuongezeka kila siku katika soko. Tablet zinazotumia Android zinapatikana kuanzia dola za kimarekani 199 (takribani Tsh 299,000/=)
Tutawaletea habari zaidi pale kampuni ya Apple itakapotoa habari kamili kuhusu jambo hili.
No Comment! Be the first one.