Google wamewezesha utafuta mraisi wa simu yako kupitia mtandao wao wa utafutaji wa Google Search, yaani Google.com.
Kama utakuwa umeunganisha simu yako ya Android na akaunti yako ya Google/Gmail basi usihofu utaweza kujua mtaa/mahali ilipo hii ikiwa ni pamoja na kuipigia au ‘kubipu’ kwa urahisi kupitia kwenye kompyuta au tableti yako.
Ukienda eneo la utafutaji yaani Search, andika ‘Find my phone’, hiki ni kiingereza cha kumaanisha unaiambia Google ikutafutie simu yako. Ukiandika na kubofya pa kutafuta katika matokeo ya utafutaji eneo la juu utaona muonekano kama huu hapa chini.
Hakikisha ume ‘log in’ kwenye Google, kwani kama hujafanya hivyo watakutaka ufanye hivyo. Kama una simu zaidi ya moja za Android zinazotumia akaunti yako ya Gmail basi watakutaka uchague simu kupitie eneo wanalokuonesha aina za simu. (Angalia picha hiyo juu).
Kama umewezesha chaguo la ‘Location’ kwenye simu yako basi pia utaweza kuona kupitia ramani ya Google Maps mahali simu hiyo ilipo. Hii inaweza ikawa ni mtaa na kama ukiangalia kwa undani unaweza kuona hadi jengo husika simu hiyo ilipo. Lakini kikubwa zaidi ni kwamba utaweza kujibipu, yaani kuipigia simu hiyo kwa kubofya eneo la ‘Ring’.
Huu ni muendelezo wa hatua wanazozifanya katika kurahisisha wewe kupata simu yako pale unapokuwa uioni ikiwa ni sababu umesahau ulipoiweka au kuna mtu ameificha au kuiiba. Kwa uwezo mkubwa zaidi kama vile kufuta data za simu ilyoibwa na ata kuifunga (yaani ‘lock’) itabidi utumia mtandao wa wao wa Android Device Manager. Muwezesho huu wa kutafuta simu yako kupitia Google Search ni kama maboresho zaidi kwani ndiyo sehemu ya kiurahisi zaidi kulinganisha na mwanzo ambapo ingekubidi ufungue mtandao wa Android Device Manager.
- Kusoma kwa undani kuhusu Android Device Manager bofya kusoma katika makala yetu hii -> Mbinu Ambazo Huenda Huzijui Katika Google PlayStore!
- Na pia unaweza kujifunza mbinu mbalimbali za kulinda simu yako zaidi kwenye makala hii -> Jinsi ya Kudhibiti Simu Yako
Kumbuka kusambaza makali uzipendazo kutoka TeknoKona kwa ndugu na marafiki! Endelea kutembelea mtandao namba moja wa habari za teknolojia Tanzania!
No Comment! Be the first one.