Apple wamekua wakijiongeza katika bidhaa zao za iPhone tofauti na makampuni mengine makubwa ambayo yapo katika soko la kutengeneza na kuuza simu.
Habari zinazozagaa sasa hivi ni kwamba kampuni hiyo nguli ina mpango wa kuja na iPhone ambayo haina tundu la kuwekea chaji, japokua hili bado hawajilithibitisha.
Kumbuka walianza kutoa vitu kadhaa katika simu zao.. walianza na kutoa ‘Home Button” kama unakumbuka, kisha wakafuata na tundu la waya wa masikioni (earphones).
lakini mara zote ambazo wanatoa baadhi ya kipengele katika simu zao mara nyingi huwa wanakuja na mbadala kwa mfano walivyoa tundu la earphone walikuja na bidhaa nyingine ijulikanayo kama Airpods.

Kama ilivyo kawaida yao wakianzishaga kitu mara nyingi makampuni mengine huja na kuiga teknolojia hiyo kwa kasi sana, kwa sasa makampuni mengi ya simu na yenyewe yamekuja na yteknolojia hiyo ya kuwa na spika za masikioni ambazo hazina waya (wireless)
Ukiachana na hayo sasa, unaweza ukajiuliza kuwa kuna faida gani ya kutoa vipengele hivyo katika simu?
Faida ni kwamba Apple inakuwa na uwezo mkubwa wa kucheza na umbo la simu, kwa mfano walivyotoa ‘home button’ wakapata wigo mpana wa kuongeza ukubwa wa kioo.. vitu kama kuondoa tundu la spika za masikioni ni kwamba vitu kama ukubwa wa betri n.k vinaweza ongezwa.

Ni kweli kabisa kwamba tundu la chaji ni moja kati ya kipengele kikubwa sana katika simu yeyote, tangia zamani simu zote zimekua zikija na teknolojia hii.
Bado inajulikana kwa kampuni ya Apple baadhi ya simu zake za iPhone zina teknolojia ya kuchaji bila kutumia waya (wireless charging). Ubaya wake ni kwamba vifaa hizo vinauzwa tofauti na simu.. inamaana havipatikani ndani ya boksi la simu.

Fununu zinasema kwamba kama simu hizo mpya za iPhone zitatoka hiyo inamaanisha kwamba ni lazima kifaa cha kuachajia bila waya kitakuwa katika boksi la simu.
lakini kwanini wanatoa kipengele hichi, pengine sababu ni ile ile ya kutaka kupata uwaja mkubwa wa kufanya mambo mengi zaidi.

Vile vile sababu za kuondoa matundu matundu haya katika simu inaweza hata ikawa ni kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia simu huingia maji (water resistance).
Simu za Apple ambazo zipo sokoni kwa sasa zenyewe zina kiwango na kiwango cha kina, yaani ukizidiaha kina fualani maji yataweza kuingia ndani na kuaharibu simu kama kawaida.
Kama Kweli Apple watakuja na hili ni wazi watatuweka wazi kwa sababu katika matamasha yao ya utambulizi wa vifaa huwa wanatangaza vifaa au vipengele vipya na vile vile wanaelezeaga sababu juu ya kwanini wamekuja na vifaa au vipengele hivyo.
Labda nikuulize, wewe unaonaje je kutakua na sababu nje ya hizo tajwa hapo juu ukiagalia tundu la chaja lilivyokuwa na umuhimu? Ningependa kusikia kutoka kwako.. Niandikie hapo chini katika uwanja wa maoni.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
No Comment! Be the first one.