Baada ya iPhone 16 na sasa simu ya Google Pixel 9 Pro nayo yapigwa marufuku kuuzwa nchini Indonesia.
Hii ni kutokana na kushindwa kwa makampuni ya Apple na Google kukidhi viwango vya maudhui ya ndani – ambapo kuna vigezo vinavyohitaji angalau asilimia 40% ya utengenezaji wa simu husika, ikijumuisha vipuri na programu endeshaji, kutengenezwa ndani ya nchi hiyo.

Hatua hii inalenga kuhimiza utengenezaji wa ndani na kupunguza utegemezi wa teknolojia ya kigeni. Serikali ya Indonesia inasisitiza kuwa makampuni ya kimataifa yanapaswa kushirikiana na wazalishaji wa ndani ili kukidhi viwango vya hivyo..
Kwa sasa, simu za iPhone 16 na Pixel 9 Pro hazipatikani rasmi nchini Indonesia. Hata hivyo, simu hizi zinaweza kununuliwa nje ya nchi na kuingizwa nchini Indonesia, lakini zitakabiliwa na ushuru mkubwa wa forodha na taratibu zingine.
Hatua ya serikali ya Indonesia ya kuzuia uuzaji wa iPhone 16 na Pixel 9 Pro ni ishara ya kuongezeka kwa ulinzi wa viwanda nchini.
No Comment! Be the first one.