Kampuni ya Apple watengenezaji wa simu za iPhone, kompyuta za Mac na tableti za iPad wamealika waandishi wa habari tarehe 12 mwezi huu katika mji wa San Fransisco huko Marekani katika kile watafiti wengi wanasema itakuwa ni kuitambulisha simu mpya ya iPhone 5.
Kumekuwa na uvumi wa picha nyingi zinazotambaa kwenye mitandao ya intaneti kuionesha iPhone 5 lakini hapo tarehe 12 uhakika utapatikana kuwa ipo vipi. Baadhi ya picha zilizovuja tunaziweka hapa, ila usisahau kurudi tena tutakapopata habari kamili hapo tarehe 12 kujua ukweli ni upi.
No Comment! Be the first one.