Mpaka sasa, tetesi kuwa Apple wameamua kuondoa kitundu cha ‘earphone’ katika simu zake mpya za iPhone 7 ambazo huenda zikatoka mwishoni mwa mwaka huu, zimeshika kasi kubwa na kukamata masikio ya mashabiki wengi wa simu hizi.
Zaidi ya mashabiki Laki Mbili duniani kote, wameungana na kutia sahihi katika mijadala iliyopo katika mitandao tofauti, kuishinikiza kampuni ya Apple kupiga chini mpango huo.
Japo mpaka sasa hakuna mbacho tayari kimethibitishwa na kampuni hiyo, lakini mitandao maarufu ikiwamo ule wa wasambazaji wakubwa kutoka China, imethibitisha ujio wa dizaini hiyo mpya ya simu, huku ikiambatana na utambulisho wa aina mpya ya Earbuds na Earphones ambazo hazitategemea nyaya kuunganishwa na simu, bali Bluetooth.
Sababu kubwa ya kutelekeza kitundu icho cha Earphone inaelezwa kuwa ni uwembamba zaidi wa iphone 7, ambao huenda ukakwamishwa kama kitundu icho kama kitaendela kuwepo. Mpaka Makala hii inapanda hewani, zaidi ya mashabiki 227,840 walikuwa tayari wametia sahihi kupinga mpango huu.
Apple wamedhamiria kuja na aina mpya ya Earphones na Earbuds zisizotumia waya ili kuunganishwa kwenye simu za iPhone. Hii inamaanisha, itabidi kuchaji earphone zako au earbuds kabla ya kutumia.
Mtandao wa 9to5Mac unaripoti kuwa, inategemwa kuwa vifaa hivyo vipya vitakuwa na uwezo wa kuondoa kelele za nje, kuwa na microphone zake, uwezo wa kupiga na kupokea, pamoja na kuiamuru SIRI kwa dhamira tofauti.
Pia huenda Earbuds hizo zikaja kwa saizi tofauti, kutegemeana na ukubwa wa masikio ya mtumiaji, mfumo ambao pia unatumiwa sana na Motorola na Bragi.
Mtandao huu wa kuaminika pia umeripoti kuwa, Apple tayari wamefanya majaribio ya makasha ya aina tatu tofauti kwa ajili ya iPhone 7, ambayo yote hayana uwezekano wa kuwepo kwa kitundu cha Eraphones, hivyo kuchocheza zaidi ujio wa Earbuds na Earphones mpya zisizotumia nyaya.
Chanzo: AppAdvice, TheNextWeb
No Comment! Be the first one.