Sticker ni vitu vya kawaida sana katika mitandao ya kijamii, hata katika mtandao wa kijamii maarufu wa WhatsApp huduma hii inapatikana.
Lakini vipi kuhusiana na kutengeneza Sticker zako mwenyewe katika mtandao huu wa kijamii (WhatsApp)? Hilo kwa sasa linawezekana kwa watumiaji wa iOS pekee na ni kuanzia iOS 17 na kuendelea.
WhatsApp imeweka mfumo huo ili kuhakikisha kwamba watumiaji wa sticker katika vifaa vya iOS (kwa sasa) wana uwezo wa kutengeneza sticker zao wenyewe.
Ili kuweza kufanikisha hili katika kutengeneza sticker zako unaweza kufanya hivyo kwa kuingia katika eneo la sticker na kisha chagua Create Sticker.
Baada ya hapo unaweza ukachagua picha yoyote unayoitaka na kisha unaweza endelea kuhariri (edit) sticker hiyo kwa kuongeza maneno, kubadilisha ukubwa, kuchora juu yake n.k.
Vile vile unaweza Hariri (edit) sticker ambayo tayari ipo, kufanikisha jambo hili itakubidi uiguse sticker husika kwa muda mrefu mpaka neno edit sticker litokee.
Kumbuka kwa upande wa WhatsApp Web tayari huduma hii imewafikia lakini ni vuziri zaidi kufanyia jambo hili katika simu sio?
Kingine ambacho wengi hakiawafurahisha ni kwamba katika WhatsApp Web utakua na uwezo wa kuhariri (edit) tuu lakani hautakua na uwezo wa kutengeneza ya kwako mwenyewe tokea mwanzo.
Kwa sasa hili limeanza kwa watumiaji wa iOS na WhatsApp Web pengine kwa watumiaji wa Android pengine watapata kipegele hiki huko mbeleni.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je ushaanza kutumia mfumo huu wa kutengeneza sticker hizi? Au unausubiria kwa hamu ili uuanze kuutumia?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.