Kwa muda mrefu kumekuwa na imani kwamba moja ya njia ya kutunza chaji ya simu yako ni kwa kuhakikisha kwamba hakuna app ambazo zinafanya kazi na wewe hauzitumii, hi ni kweli lakini ni kwa watumiaji wa Android tuu na sio watumiaji wa iPhone.
Imani kwamba ukifunga app ambazo zinajiendesha katika background ya simu yako imekuwapo kwa muda mrefu sasa na ni watumiaji wengi sana wa simu zote zikiwamo iPhone wamekuwa wakiitumia njia katika harakati za kupunguza matumizi ya chaji za simu zao.
Mwanzoni mwa wiki hii mtumiaji mmoja wa iPhone aliamua kumuandikia Mtendaji mkuu wa Apple bwana Tim Cook na kumuuliza juu ya swala hilo, bosi huyo wa Apple hakujibu swali hili lakini makamu wa raisi wa uhandisi wa software alilijibu swali hilo.
Mtumiaji huyo aliuliza iwapo Tim Cook huwa anafunga app zilizo katika background na iwapo zoezi hilo linasaidia katika uhifadhi wa chaji ya betri, swali hilo lilijibiwa na makamu wa raisi wa uhandisi wa software kwamba hapana na hapana yaani bosi huyo alisema kwamba huwa hafungi app zilizo katika background na pia kufunga hakusaidii uhifadhi wa chaji ya simu.

Majibu hayo ya ni ya kuaminika na kwa ujumla yameondoa tetesi zote tulizokuwa tunazijua ama kuzisikia juu ya kuzima app zinazofanya kazi katika background.