iPhone ya kwanza kabisa ilitambulishwa Rasmi mwaka 2007 na Steve Jobs na huu ndio ulikua mwanzo wa iPhone zote mpaka sasa.
Kwa 2007 iPhone ya 4GB ilikua ikiuzwa kwa dola za kimarekani 500 huku ile ya 8GB ikiwa inapatikana kwa dola za kimarekani 600.
Lakini kingine ni kwamba hili sio la kushangaza sana yaani bidhaa za zamani kuanza kuuzwa katika minada kwa gharama kubwa zaidi kwa sasa.
Lakini hapa cha kushangaza ni kwamba ile ya 8GB iliuzwa katika mnada kwa dola za kimarekani 63,000 na hii ilikua ni hela nyingi sana maana mnada huo ulianzia kwenye dola za kimarekani 2,500.
Wakati ukidhani hiyo ni pesa kubwa sana hii ya GB 4 inaweza ikakushangaza zaidi maana maana imeuzika zaidi ya mara tatu ya gharama ya hiyo ya mwanzo ambayo iliuzwa mwezi februari.
iPhone ya 4GB iliwekwa rasmi kwenye mnada mwezi uliopita (juni) tarehe 30 na kianzio chake kilikua ni dola za kimarekani 10,000.
Kwa haraka haraka wengi walizania hata simu hiyo ikiuzika basi itakua imeuzika kwa kiasi cha dola za kimarekani 50,000 pengine mpaka kufikia 100,000.
Cha kushangaza ni kwamba mambo yalikua yanaenda taratibu tuu mpaka bei kufikia dola za kimarekani 42,000 na baada ya hapo mambo yakabadilika kabisa.
Mpaka sasa ni kwamba simu hiyo imeuzika kwa dola za kimarekani 190,372.80 na hili ni wazi kwamba limewaacha watu wengi midomo wazi.
Mara kwa mara makampuni mengi wamekua wakiwa na tabia hii ya kuuza katika mnada bidhaa zao za zamani ambazo ziliacha alama kwa watu.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.