Katika swala zima la simu, watumiaji huwa na katabia ka kupenda kubadilisha na kwenda katika toleo lingine la simu pale linapotokea.
Kwa mfano mtu anaweza akatoka kutumia Samsung Galaxy s4 na kwenda kutumia s5 pale itakapoingia sokoni. Swali lililopo je ni kwa haraka gani mtu anaweza akabadilisha simu hiyo? Labda nikuulize wewe ni muda gani unachukua kubadilisha simu janja yako? Je ni mara kwa mara kila toleo jipya likitoka?
Tafiti nyingi zimefanyika na watu waliobobea katika teknolojia na utafiti, jibu walilokuja nalo ni kwamba watumiaji wengi wa iPhone (Apple) huwa wanasubiria muda mwingi ili kubadilisha vifaa vyao kwenda katika matoleo mengine ukilinganisha na watumiaji wengine kama wale wa Android.
Hii ni kweli kabisa kwani ukiangalia kwa jicho lingine ni kwamba – cha kwanza kabisa simu za iOS vina bei ya juu kidogo ukilinganisha na vifaa vingine – kampuni huwa linaachia simu mpya kila mwaka na hii mtu unaweza ukasema kuwa ni moja kati ya sababu ambazo zinaweza zikamfanya mtumiajia wa iOS kukaa sana bila kubadilisha kifaa chake.
Kampuni ya Apple ina tabia ya kufanya mabadiliko madogo kwa mwaka mmoja na kufanya mabadiliko makubwa kwa mwaka unaofuata. Yaani ni hivi, mwaka huu wanaweza kwa mfano kama mwaka huu wana iPhone 5 basi mwakani watatoa iPhone 5s. Na mwaka unaofuata watafanya mabadiliko makubwa na kutoa iPhone 6.
Kwa namna moja au nyingine kama mtumiaji atakuwa akitumia iPhone 5 anaona haina haja kubwa ya kubadilisha kwenda katika 5s bali atasubiria mpaka kufikia katika iPhone 6.
Kingine kikubwa ni kwamba programu endeshaji inachukua nafasi kubwa sana katika swala hili. Kwani inayotimika sana ni ile ya Android.
Hili ni jambo zuri lakini kuna kipindi linaweza likaja kuathiri kampuni ya Apple kama wateja wake wanakaa muda sana mpaka kuja kubadili simu zao kwenda kwenye matoleo mapya.
Kwa mwaka 2017 lazima utakuwa ni mwaka mzuri kwa Apple. Kumbuka unakuwa ndio mwaka mzuri kwani unakuwa na maboresho makubwa na hii ni kutokana na simu za iPhone 7 na iPhone 7 plus. Ukiachana na kuwa ni mwaka wa maboresho makubwa pia tumeona simu za Samsung Note 7 zikilipuka katika himaya ya watumiaji.
Ukiachana na haya yote ukweli ni kwamba watumiaji wengi wa Android huwa wanatumia muda mchache sana katika kuhakikisha wanajipatia toleo jipya kabisa la simu janja wanazotumia na hii ni tofauti kabisa na watumiaji wa iOS.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment. Je na wewe huwa unabadilisha simu mara kwa mara na kwenda katika toleo jipya, Vile vile unatumia simu ya aina gani? Android, iOS au ___?