Watu wengi hupenda kutumia mbadala wa programu halali ya WhatsApp, hizi programu mbadala huitwa “WhatsApp Mods” zipo za aina nyingi kama GBWhatsApp, FMWhatsApp, WhatsApp Plus, WhatsApp Go n.k, ni ukweli kwamba kutumia mbadala wa WhatsApp yaani kutumia WhatsApp mods unaweza kufanya mambo ambayo Whatsapp ya kawaida haiwezekani kufanya kama vile;
• Kuweka “status” kuwa ndefu yaani unaweza kuweka video mpaka ya dakika 5.
• Uwezo wa kuficha last seen, yaani unaweza kuondoa ule mda mara ya mwisho kuonekana kwenye WhatsApp.
• Uwezo wa kuona status ya mtu pasipo yeye kuona kama umeangalia hiyo status yake.
• Uwezo wa kusoma jumbe/messages zilizofutwa.
• Uwezo wa kuzuia “view once” (hali ya mtu kutuma picha au video ambayo itakulazimu uione mara moja tu)
Kuna mambo mengi amabayo unaweza kuyafanya kwenye hizi programu mbadala wa WhatsApp yaani “WhatsApp Mods” lakini Je, ni salama kwako kutumia ?
Kiuhalisia mbadala wa WhatsApp ya kawaida yaani hizi “Whatsapp Mods” sio program nzuri kutumia kama unajali taarifa zako muhimu kukuhusu wewe, kwa sababu hizi programu mbadala wa WhatsApp ya kawaida zinawekewa kitu kinaitwa “programu hasidi” yaani wadudu/viruses kwa ajili ya kazi flani maalumu.
Kuna kirusi kipo kinaitwa “triada mobile trojan” ambacho kinapatikana Kwenye FmWhatsapp , GbWhatsapp na kinashambulia simu yako na kudukua taarifa zako muhimu kuanzia kusoma sms, kuona namba zako zilizo kwenye simu, kukuletea matangazo kila mara pia kuuza taarifa zako.
Hizi programu mbadala wa WhatsApp yaani “Whatsapp Mods” hazina ulinzi wa kutosha kulinda mawasiliano yako yaani haina “end to end encryption” maana yake mawasiliano yako baina ya mtu na mtu hayafichwi (encrypted) ukilinganisha na programu halali ya WhatsApp.
Kubwa zaidi ni kwamba namba yako (akaunti yako) ya WhatsApp inaweza kuzuiliwa kutumia WhatsApp ya kawaida (banned) na hii ndiyo sababu kubwa namba nyingi zimezuiliwa kutumia WhatsApp ya kawaida, ni sababu ya matumizi ya programu mbadala na WhatsApp.
Ni ngumu kufanya chelezo ya taarifa (data backup) kwa kutumia programu mbadala wa WhatsApp,
No Comment! Be the first one.