Wachambuzi wengi sasa waliofanikiwa kuona matoleo mapya ya simu za Samsung Galaxy (S6 na S6 Edge) huko mji wa Barcelona, Uhispania wameonekana kuzoza kwamba simu hizo mpya za Samsung zinafanana sana na zile za iPhone, toleo la sita.
Kampuni zote mbili zina historia ndefu ya kupelekana mahakamani kwa kuibiana ubunifu ila sasa inaonekana Samsung wenyewe wameamua kuonesha bila kujificha kwamba wanaelekea kukubaliana na baadhi ya vitu vya kibunifu kutoka kwa Apple kwenye nyanja ya simu za mkononi.
Eneo la iafoni:
Sasa kishimo cha iafoni (earphone jack) kinapatikana chini ya S6 kama ilipokuwa muda mrefu kwenye iPhone, pengine ili ikurahisishie usigeuze simu unapoitoa mfukoni mwa suruali au labda kuweka sehemu za sauti inapotoka pamoja (karibu na spika)?
Eneo la Spika na ukubwa wake.
Spika ya Samsung sasa ina uwezo mara 1.5 zaidi ya ilivyokuwa kwenye S5! Na kikubwa zaidi, sauti haitafichwa utakapoilaza Samsung hii mpya popote, hata kwenye kitanda au hata kwenye mfuko ambapo mlio wa simu utasikika bila shida. Simu za iPhone zimekuwa zikitengenezwa hivi kwa muda sasa.
Dizaini ya Mwili Usiogawanyika wa Alumini.
Samsung wameona pengine plastiki humfanya mtu adhani simu ya Samsung Galaxy haina hadhi ya juu na baadala yake wameamua kufuata dizaini ya iPhone yenye chuma cha alumini na kwa kufanya hivyo, imewabidi kuondoa uwezo wa kutoa betri na kuongeza hifadhi kwa memori-kadi, pengine wakikubalina kwamba soko linaelekea zaidi kwenye hifadhi-pepe. Lakini pia wamedai sababu kubwa ya kuachana na suala la memori-kadi ni ukweli wa kuwa watumiaji wengi wa simu hawatumiagi zaidi ya GB 25 na kuhakikisha wanakidhi haja za wote simu zao zinapatikana kwenye ukubwa diski-uhifadhi wa GB 32, 64 au 128
Batani ya Kurudi Nyumbani (Mwanzo).
Muongozo wa Androidi kutoka Google unaelekeza kampuni za simu kutumia batani ya mwanzo isiyo ya kubonyezeka kama ilivyo kwenye simu za Sony na LG ambazo zina batani hii kwenye skrini. Samsung wao hufanya tofauti na wanasema wanafanya hivi kwa sababu ya teknolojia ‘finger-print recognition’ amabayo kwa sasa wanaiamini zaidi katika batani wanazotumia.
Samsung wanajiteteaje?
Samsung wanasema wamewasikiliza sana wateja wao kwa kuangalia soko linavyoenda, na ukiangalia, soko linasema kwamba iPhone zimetamba zaidi. Je kwa mtazamo wako ni kweli simu hizi zimafanana sana?
SamsungTZ wanaleta lini simu hizi?
Haijulikani kwa kweli. Katika nchi za nje, Samsung wanategemea kuanza kuuza simu hii mwanzoni mwa April mwaka huu ila kwa hapa nyumbani tutegemee kupata Samsung Galaxy S6 na S6 Edge baada ya miezi mitatu kutoka sasa au ndani ya miezi minne ukizingatia muda uliochukua kwa SamsungTZ kuleta Galaxy Note 4.
Unaweza pia kutazama video hii ya mmoja wa viongozi wa Samsung akielezea BBC kuhusu dizaini ya Samsung mpya – Samsung/ BBC
Picha Na: phonesltd.co.uk , gottabemobile.com, imore.com.
No Comment! Be the first one.