DropBox ni njia nzuri ya kuweza kuwa na data zako kama mafaili ya ofisi, picha, video au muziki, iwe ofisini, nyumbani, dukani au popote ulipo, muda wowote. Mara nyingi katika ulimwengu wa sasa tunakuwa kwenye mishemishe na mara nyingi tunajikuta tumesahau kubeba vitu tunavyotakiwa kuwa navyo. Hii hali inatufanya tuwe na perfomance ndogo katika vitu muhimu na mara nyingi inatubidi tupoteze muda na pesa kufuata au kufuatilia vitu hivyo muhimu. DropBox inatuwezesha na inasaidia kupunguza aibu au adha hiyo.
DropBox inakurahisishia maisha. Kwa kutumia DropBox hautakuwa na ulazima wa kubeba laptop huku na kule, kwani ukiwa ume’install DropBox kwenye computer ya nyumbani, kazini na hata simu faili lolote utaloliweka utaweza kulipata sehemu zote hizi. DropBox itakuwa inali’copy kwenye account yako online na kulikopi tena kwa njia ya kulidownload kwenye folder lako la DropBox kwenye kifaa chako kingine.
DropBox inakupa nafasi zaidi ya kuweka vitu vyako na pia ‘back-up’ pale vifaa chako cha data kinapoharibika au kuibwa. Unapoanza na DropBox, unapewa 2GB za kuweka data zako inayoweza kufikia mpaka 18GB kwa kusaidia kuieneza DropBox kwa ndugu, jamaa na marafiki. Pia, unaweza kununua nafasi zaidi na huduma ya ‘DropBox for Teams.’ Kuna njia nyingine nyingi ambapo DropBox inaweza kurahisisha maisha yako. DropBox inakupa uwezo wa kumualika mwenzako kutumia faili unalokusdia katika akaunti yako huku mafaili mengine yakibaki ya kwako tu kuona na kutumia. Kwa kutumia huduma hii, wewe na ndugu, rafiki au mfanyakazi mwenzako mnaweza ku’share’ data na kuweza kufanya kazi pamoja.
Kiufupi, DropBox ni njia rahisi na salama ya kuongeza perfomance katika ulimwengu wa sasa unaoonesha mwitiko mkubwa wa kurahisisha maisha kwa kutumia computer, smartphones na tablets na mfumo wa ulimwengu wa intaneti. Unaweza sasa kujiunga na DropBox kwenye www.dropbox.com kwenye kifaa chako kinachotumia intaneti na kufaidi huduma hii.
One Comment