SoundCloud pamoja na Sony Music ni makampuni makubwa tuu yanayojishughulisha na maswala mbalimbali ya muziki. Kizuri ni kwamba wawili hawa wameingia katika makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja
Hapa lebo hii ya muziki (Sony Music) imetengeneza dili na kampuni kubwa inayojihusisha na mambo ya kusikiliza na kuangalia muziki kupitia mtandao (Streaming).
Siku hizi njia hii (stream) imekua ndio kila kitu kwani makampuni mengi kama bado hayana huduma hii yanafikiria kuwa na huduma hii. Hata mtandao mkubwa wa kijamii wa Facebook kwa sasa wana huduma hii lakini wao wamejikita katika kuoyesha video mtandaoni.
Dili la Sony Music Na SoundCloud ni kwamba mtandao wa SoundCloud uweke mazingira ya wasanii kutoka Sony waweze kuweka miziki yao katika mtandao huo. Ishu kubwa ni SoundCloud kuwapa leseni (Sony Music) ili wasanii wao waweze kuweka miziki yao hapo. Kwa kufanya hivyo basi SoundCloud itaanzisha huduma ya kujiunga kila baada ya muda Fulani (subscription) ili kutumiza hili katika mwaka 2016.
Jambo hili lilikuwa likitegemea kwa muda mrefu tuu, lakini mambo yalipamba moto mwaka jana baada ya kampuni la Sony Music kuitaka SoundCloud itoe miziki ya wasanii wake katika mtandao huo.
Dhumui kubwa kwa kufanya hivyo ni kuhakikisha kwamba kila kitu kinaenda kisheria na faida inaonekana kama inavyostahili pindi tuu watakapo anzisha huduma hiyo ya malipo ya kila baada ya muda (subscription), maara nyingi kila baada ya mwezi.
Hii sio mara ya kwanza kwa SoundCloud kupata dili kubwa kama hili kutoka kwa kampuni kubwa linalojihusisha na muziki. Awali SoundCloud ilipata dili na kampuni la Warner Music Group (WMG) na hata Universal Music Group (UMG). Kwa kipindi hicho kampuni la WMG ndio lilikuwa la kwanza kupata dili hilo nah ii inasemekana ni kwa sababu kiongozi mmoja wa WMG kwa kipindi hicho alikuwa na wadhifa mkubwa katika kampuni ya SoundCloud kwa hiyo kwa namna moja au nyingine aliweza kurahisisha kutokea kwa dili hilo.
Mzigo mkubwa bado unabaki katika kampuni la SoundCloud kwani imekua ikipata faida ndogo kulingana na namba ya watumiaji wa mtandao huo. Inawabidi waje na njia madhubuti ambazo zitawasaidia katika kuhakikisha wao wanaridhika na wenzao wa Sony Music wanaridhika pia
Bado haijafahamika ni njia gani kampuni la SoundCloud litatumia kuhakikisha linagawa faida inayoptakina kwa makampuni matatu (Warner Music Group, Universal Music Group na Sony Music) ambayo yana dili na kampuni hiyo.