Kuwa na blue tick karibu na jina lako la mtumiaji kwenye mitandao ya kijamii ni jambo kubwa. Inaonyesha kwamba akaunti yako imethibitishwa na ni ya kweli, iwe akunti yako ni ya brand, mtu maarufu, au hata timu ya michezo. Uthibitisho huu unasaidia wafuasi wako kujua kuwa wanawasiliana na chanzo halisi, na si akaunti ya parody au mashabiki.. Hii ni blue tick ambayo TikTok inatoa ili kukusaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu maudhui unayotazama au akaunti unazofuata.
Blue Tick ni Nini?
Blue tick inamaanisha akaunti imethibitishwa kuwa ni mali ya mtu au brand inayoisimamia. Hii ina maana unaweza kuwa na uhakika kwamba akaunti zilizothibitishwa ni za watu au brand halisi, badala ya akaunti za parody au mashabiki. Kama mtayarishaji wa maudhui, blue tick husaidia kujenga uaminifu na wafuasi wako.
Jinsi ya Kutambua Akaunti Iliyothibitishwa
Blue tick ni alama ya tiki ya bluu inayojitokeza karibu na jina la mtumiaji kwenye akaunti ya TikTok. Ikiwa akaunti haina blue tick karibu na jina la mtumiaji lakini inaonyeshwa mahali pengine kwenye wasifu (kama vile bio), hiyo si akaunti iliyothibitishwa. Ni TikTok pekee inaweza kuweka blue tick.
Jinsi ya Kupata Uthibitisho Kwenye TikTok
Unaweza kukamilisha ombi la uthibitisho wa TikTok ili kuzingatiwa kwa blue tick. TikTok huzingatia mambo kadhaa kabla ya kutoa blue tick, kama vile kama akaunti ni hai, ya kweli, maarufu, na ya kipekee. Hatuzingatii idadi ya wafuasi au likes kwenye akaunti.
Mahitaji ya Akaunti kwa Uthibitisho
- Active: Akaunti yako lazima iwe imeingia kwenye TikTok ndani ya miezi 6 iliyopita.
- Authentic: Akaunti yako inawakilisha mtu halisi, biashara, au chombo.
- Complete: Akaunti yako lazima iwe ya umma na iwe na wasifu uliokamilika wenye jina la mtumiaji, bio, picha ya wasifu, na angalau chapisho moja.
- Notable: Lazima uwe umeangaziwa katika vyanzo vingi vya habari. Hatuzingatii taarifa kwa vyombo vya habari na vyombo vya habari vilivyofadhiliwa au vilivyolipwa.
- Secure: Akaunti yako lazima iwe na uthibitisho wa hatua 2 (two-step verification) na barua pepe iliyothibitishwa. Hii inahakikisha akaunti inabaki kwa mmiliki halisi na ni salama dhidi ya wahusika wabaya.
Jinsi ya Kuomba Uthibitisho Kwenye TikTok
Ili kuomba uthibitisho wa akaunti yako ya TikTok:
- Fungua app ya TikTok, gonga Profaili chini.
- Gonga kitufe cha Menyu ☰ juu, kisha chagua Mipangilio na faragha.
- Gonga Akaunti.
- Gonga Verification.
- Gonga Start, kisha fuata hatua za kuwasilisha ombi la uthibitisho.
Ikiwa hujapewa blue tick baada ya kupitia ombi lako, unaweza kuwasilisha ombi jingine baada ya siku 30 baada ya kuarifiwa.
Gharama za Kupata Uthibitisho
Hatutozi gharama yoyote kwa kupata uthibitisho. Chombo chochote kinachodai kuuza uthibitisho wa TikTok hakihusiani na TikTok.
Kwanini TikTok Inaweza Kuondoa Uthibitisho?
TikTok inaweza kuondoa blue tick wakati wowote na bila taarifa. Sababu za kuondoa zinaweza kujumuisha:
- Akaunti kuhamishiwa kwa mmiliki mwingine.
- Jina la mtumiaji kubadilishwa.
- Aina ya akaunti kubadilishwa kati ya biashara, binafsi, au taasisi.
- Akaunti kukiuka Miongozo ya Jamii (Community Guidelines) na Masharti ya Huduma (Terms of Service) mara kwa mara au kwa ukali.
Kwa kuzingatia haya yote, blue tick inasaidia kujenga uaminifu na uwazi ndani ya jamii ya TikTok, na kuhakikisha kuwa maudhui na akaunti unazozifuatilia ni za kweli
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
No Comment! Be the first one.