SnapChat ni moja ya app inayopata umaarufu kwa kasi sana kwa sasa. Makala hii inalenga kumsaidia mtu kujua jinsi ya kujiunga na kutumia app ya Snapchat.
Pakua na kisha Install Snapchat.
Snapchat inapatikana katika masoko ya application ya Android na iOS bure, ipakue na kisha install katika simu yako. ukifungua hii app utaweza ku log in ama kama hauna kabisa akaunti utatakiwa kutengeneza akaunti kwa kuingiza habari zako kama vile anuani ya barua pepe password na tarehe ya kuzaliwa (App hii inaruhusu watumiaji walio na umri wa kuanzia miaka 13).
Baada ya kujisajiri na kutengeneza akaunti yako Utatakiwa kuingiza namba ya simu yako kwaajiri ya kuthibitisha kwamba wewe ni mtu kweli, hapa utachagua nchi yako uliyopo (TZ-Tanzania) kisha utaandika namba yako ambapo utachagua namna ya kuthibitishwa kama ni kwa kutumiwa ujumbe wenye namba au kupigiwa simu kutajiwa namba hizo za kuthibitishwa.
Baada ya kuthibitishwa Snapchat itaomba kuweza kutumia namba za simu zako ulizohifadhi katika simu yako kwaajiri ya kukuonesha marafiki zako ambao wapo katika mtandao huu.
Jinsi ya kutumia.
Snapchat ina sehemu kuu tano ambazo ndio zinatumiwa kufanya mambo mengi zaidi, ukiweza kuzielewa sehemu hizi tano basi utakuwa umeweza kutumia Snapchat bila ya shida yeyote ile.
Sehemu ya I
Huu ni ukurasa ambao unafunguka pindi unapofungua Snapchat, hapa unaweza kupiga picha ama kurekodi video yako.
Kupiga picha: Picha inapigwa kwa kugusa kitufe cha duara kilicho katikati upande wa chini, uunatakiwa kuchagua kama unatumia kamera ya mbele ama ya nyuma ya simu yako kwa kugusa kipicha cha kamera juu kulia na pia unaweza kuwasha ama kuzima flash kwa upande wa juu kushoto.
Kurekodi video:Video inarekodiwa kwa kushikilia kitufe cha katikati upande wa chini ambacho ni chaduara, kwa kushikilia kitufe hiki video itakuwa inaendelea kurekodi.
Ukimaliza kupiga picha ama kuchukua video basi utakuwa katika ukurasa wa kui edit picha ama video yako na hapa unaweza kufanya mambo mengi baadhi ya mambo unaweza fanya ni haya
- Kwa kusukuma picha yako kulia na kushoto utaweza kuchagua filters mbali mbali zinazopatikana.
- Unaweza kuweka emoji katika picha yako kwa kugusa kialama cha karatasi kilichopo juu kulia.
- Unaweza kuandika maandishi juu ya picha yako kwa kugusa kialama cha T ambacho nacho kipo kulia juu.
- Unaweza kuchola kwa kalamu ya rangi upendayo kwa kugusa kialama cha penseli juu kulia.
- Kama unataka kuongeza muda ambao hii picha yako itaonekana kwa kugusa sehemu yenye kialama cha duara na katikati kuna 3.
- Ukitaka kuhifadhi hiyo picha yako katika simu yako (picha zote za snapchat hazihifadhiwi katika simu kwa hali ya kawaida) basi ukibonyeza kialama cha V kilicho kushoto upande wa chini.
Kuna namna mbili unaweza kusambaza hii picha ambayo umeiremba kadiri unavyopenda, moja: kwa kumtumia mtu mmoja ambaye yupo katika orodha ya marafiki zako ama unaweza kuiweka katika kitu kinachoitwa My story Marafiki zako watakuwa wanaona hizi picha ulizoziweka katika My story moja baada ya nyingine kwa muda uliouweka wewe.
Sehemu ya II
Hii ni sehemu ya Contacts zako hapa utawaona marafiki zako wote walio snapchat na unaweza kuwaomba urafiki ambao hauna urafiki nao. Ili kufikia sehemu hii unatakiwa ku swap kwenda kulia pindi unapokuwa katika ukurasa mkuu wa Snapchat(ule ukurasa wenye kamera).
Sehemu ya III
Hii inaitwa Stories ni sehemu unayoweza kuona picha na video za marafiki zako ambazo wameweka katika kipengere cha My story.
Ili kufika katika ukurasa huu inabidi ku swap kwenda kushoto pindi unapokuwa katika ukurasa mkuu wa Snapchat (ule ukurasa wenye kamera)
Sehemu ya IV
Hapa ni kwenye ukurasa ambao unakuwa na makampuni makubwa hasa ya habari kama CNN NATIONAL GEOGRAPHIC nk. Sehemu hii inaitwa Discover na inapatikana ukiwa katika ukurasa wa Stories kwa kwenda ku gusa alama kama ya duara katika upande wa kulia juu.
Sehemu ya V
Hii ni sehemu muhimu kwa kuweza kuwaona walio ku add (mtu akikuadd ataonekana katika sehemu ya added me) na kuwaruhusu kuona snapchat yako, sehemu hii pia inaweza kukusaidia kuweza kubadili taarifa zako za msingi. Sehemu hii unafika kwa kukigusa ki alama cha Snapchat kinachokaa juu katikati ya ukurasa mkuu wa Snapchat (ule ukurasa wenye kamera).
No Comment! Be the first one.