Risiti za ujumbe kupokelewa ni alama ya kuonesha kwamba ujumbe uliotumwa umepokelewa na muhusika na huwakilishwa na alama ya vema mbili za blue maarufu kama blue ticks.
Mtumaji wa ujumbe huoneshwa alama ya vema mbili zikiwa na rangi ya bluu na hii huashiria kuwa ujumbe sio tu umemfikia mlengwa bali pia umefunguliwa, huduma hii ilikosolewa saana na wakosoaji kwa kuwa ilikuwa ikiingilia faragha ya watumiaji wa WhatsApp.
Je unachukizwa na risiti za ujumbe kusomwa!? hupendi wanao kutumia ujumbe wataarifiwe pindi unapoufungua ujumbe huo!? Kama jibu ni ndiyo basi upo mahali sahihi, makala hii itakusaidia ili uweze kuondoa risiti hizi za ujumbe kusomwa hivyo kuwaondolea uwezo wanaokutumia ujumbe kujulishwa pindi unapozisoma jumbe zao.
Kama ungependa unapofungua ujumbe uliotumiwa basi yule aliyetuma ujumbe asijue kama umeufungua basi fuata hatua zifuatazo>>> Menu —-> Account —->Privacy
1. Nenda katika menyu kuu ya simu yako na kisha bonyeza kwenda katika sehemu ya mipangilio(settings)
2.Chagua Account

3.Chagua privacy
Pamoja na mambo yote ukiwa katika kurasa hii utona sehemu iliyo andikwa read receipts ondoa alama ya pata katika kiboksi kilichopo mbele (kwa wanaotumia mfumo wa android) na kama unatumia mfumo wa iOS basi kiwashe hicho kitufe.
Angalizo hii njia haitaondoa risiti za ujumbe unaopokelewa katika makundi ya Whatsapp hii inamaana kwamba kama utafungua na kusoma ujumbe unaotumwa katika makundi basi wote walio ndani ya kundi hilo watajua muda ulioupokea ujumbe huo.
hiyo jinsi ya kujitoa kwenye group la watsApp nimetry ila imegoma kwanini??