Ngoja kwanza, hivi umesoma kuhusu Jinsi Ya Ku ‘Lock’ Kivinjari Cha Mozilla Kwa Kutumia Neno Siri (Password)? kama bado Bofya hapa. Kama unavyojua muda mwingine ni vizuri kuweka neno siri katika kivinjari unachotumia.
Hii itakusaidia na kukuhakikishia hata pale unapotoka katika mitandao yako ya kijamii bila ku ‘sign out’ kuwa taarifa zako hazitaishia kwenye mikono mibaya. Hii inamaanisha kuwa mtumiaji wa kivinjari hicho cha Google Chrome itamlazimu aingize neno siri wakati akiwa anafungua kivinjari hicho.
Jinsi Ya Kuloki Google Chrome Kwa Kutumia Neno Siri
Google Chrome inatoa neno siri kwa ajili ya kulinda taarifa za watumaiji wake. Kwa kutumia huduma hii ya usalama utaweza kuloki kivinjari chako cha google tena bila hata ya kukariri neno siri jipya/lingine kwani utatumia lile la google (lile neno siri moja kwa akaunti zote za Google). Kuweza hili fuata hatua zifuatazo
- Fungua kivinjari cha Google Chrome na Kisha andika chrome://flags katika sehemu ya kuandika tovuti kisha bofya enter
- Bofya Ctrl + F kisha andika Enable new profile management system alafu bofya enter
- Badilisha neno default na kuwa enabled katika machaguo matatu katika kibox
- Ukiangalia kwa chini utaaona neno Relaunch Now, click hapo
- ‘Sign in’ katika akaunti yako ya google kwa kubofya kialama kilicho upande wa kushoto kutoka kwa kialama cha ku ‘minimize’
- Kisha bofya menu ya Google chrome na kisha nenda katika eneo la ‘settings‘. ukiwa katika settings angalia palipoandikwa ‘People’ na kisha click Add Person
- Weka Alama ya tiki kwenye neno ‘Control and view the websites this person visits’ na kisha bofya add
- Click katika kialama cha akaunti kushoto kwa alama ya ku ‘minimize’, utaona kialama cha kuweka loki. Click sehemu hiyo ya kuweka loki mda wowote unapotaka kukiweka kivinjari chako katika hali ya usalama. Neno siri la kivinjari hiki litakuwa sawa na lile la akaunti yako ya google.
Je Njia Ya Hapo Juu Imekuchanganya? TeknoKona Inazidi Kukufumbua, Haya Twende Hii Ya Pili Na Rahisi.
Hii ni njia rahisi ya kukifanya kivinjari chako cha Google Chrome kibaki katika hali ya usalama. Kwa mfano labda ulikuwa unafanya kazi katika kivinjari chako na ukakiacha kwa dakika tano tuu, basi kivinajari kitatoa maombi ya mtu kuingiza neno siri ili kuendelea kukitumia.
- Fungua WebStore katika kivinjari chako cha google chrome na kisha andika Browser Locker au nenda moja kwa moja kwa kubofya hapa
- Click ADD TO CHROME kukiwezesha katika google chrome. Kitatokea kiboxi kikikuuliza kuhakikisha kisha bofya Add
- Mara tuu baada ya hiyo ‘Browser locker‘ kuingia katika kivinjari chako. Itakuaomba ujaze taarifa zako za neno siri kwa kutengeneza neno siri jipya.
- Baada ya kuweka neno siri jipya.. kama ukiakaa baada ya muda bila ya kutumia kivinjari chako cha Chrome basi kitaomba uingize neno siri
Kama Ukitaka Badilisha Neno Siri Fanya Haya
- Nenda katika ‘menu‘ ya chrome kisha eneo la settings
- Katika eneo la Settings, click ‘Extensions’ na itaonyesha extentions zote ambazo zimewekwa katika kivinjari hicho
- Tafuta Browser Locker na kisha bofya Options. Itakupeleka katika ukurasa mwingine ambao unaweza weka neno siri jingine/jipya na hata kuseti muda wa kuomba neno siri hilo
No Comment! Be the first one.