Unataka kujua ni vitu gani ushawahi kuvipa ‘like’, ku ‘comment’ ama kuweka katika akaunti yako ya Facebook tangu siku umejiunga? Ipo namna ya kuangalia yote hayo katika kurasa yako ya Facebook. Facebook inaweka kumbukumbu na ipo tayari kukuonesha yote uliyowahi kuyafanya katika mtandao huu wa kijamii maarufu zaidi duniani.
Kama unataka kuona mambo uliyofanya tangu ulipojiunga basi ingia Facebook kama kawaida kisha nenda katika profile yako hapo utaona sehemu imeandikwa ‘Activity Log’ bonyeza hapo kurasa nyingine itafunguka.
Huu ni ukurasa ambao ni wewe tu unayeuona na hapa ndio kuna kila post uliyowahi kuweka Facebook, kuna kila ujumbe uliyowahi kuandika pia kila na pia historia nzima ya mambo ambayo ushawahi kuyapenda (yaani ‘Like’)
Unaweza ku-chuja uone nini na nini usione kwa mfano unatafuta picha basi utachuja na post za picha pekee ndio zitatokea,ama kama unatafuta ‘post’ yako ya zamani basi weka pata katika “Your posts” na hapo utaletewa post zako zote za nyuma hadi siku uliyoanza kutuma Facebook, unaweza chuja post hizi kadili unavyopenda kama ambavyo inaonekana.
Hii inaweza kuwasaidia wale ambao wanataka kuona kitu walichowahi andika ama kulike siku za nyuma.
Je ni jambo gani jingine ungependa kujifunza kuhusu Facebook? Endelea kutembelea mtandao wako namba moja kwa maujanja na habari!
No Comment! Be the first one.