Somo la hisabati limekuwa tatizo watu wengi mashuleni na katika maisha ya kila siku. Masuala yanoyohusisha mahesabu, yamekuwa kikwazo kikubwa kwa maisha ya kila siku kwa watu wengi. Pengine wakati wa kujua punguzo la bei ya nguo fulani iliyowekwa kwa asilimia katika duka maarufu la nguo, au kujua asilimia ya punguzo kubwa la bei katika supermarket au duka lolote kubwa, mahesabu yamekuwa yakiumiza kichwa wengi.
Shukrani nyingi zinakwenda kwa iOS 9 kwa kuleta namna rahisi zaidi ya kufanya mahesabu yako.
Uwezo wa kutafuta (Search) katika iOS 9 imetokea kupendwa sana na watu wengi, tofauti na iliyokuwa katika iOS 9. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, ‘search’ katika iOS8 ilikuwa finyu na yenye uwezo mdogo wa kutafuta vitu katika simu yako.
Katika iOS 9, mambo yamebadilika kabisa. Sasa unaweza kutafuta watu, kuwapigia au kuwatumia ujumbe mfupi, kwa kutumia mfumo wa kutafuta pekee. ‘Search’ imeboreshwa mara dufu. Wakiwa wameongeza uwezo wa kufanya mahesabu rahisi na kubadili vipimo na sarafu, ni ngumu kukataa kuwa na iOS9.
FANYA MAHESABU KWA KUTUMIA SEARCH iOS 9
Ndio, app ya kikokotoo ipo kama kawaida katika iOS 9. Lakini wakati mwingine hutumia muda mrefu kuanza kutafuta app hiyo katika simu yako ili kufanya mahesabu rahisi ya muda mfupi. Sasa, kwa kutelezesha kioo chako kama unataka kutafuta kitu, utaweza kufanya hesabu rahisi kwa kutumia ‘search’ ya simu yako. Telezesha kioo chini kupata huduma ya ‘search.’

Gusa sehemu ya kutafuta katika kitufe cha kutafutia, kisha andika hesabu zako rahisi na utaletewa majibu kwa upesi zaidi katika kitufe kinachosomeka ‘Top Hint’. Ndio, ni rahisi hivyo.

Lakini ebu subiri, vipi unaweza kubadilisha sarafu au vipimo vya kilomita na maili? Ndio, kama uwezo wa kikokotoo cha kawaida kinavyoweza kukuletea majibu, ‘search’ ya iOS 9 pia inaweza kufanya hivyo. Kwa urahisi kabisa, andika kipimo cha umbali, fedha au uzito unaotaka kuubadili kwenda kipimo kingine na majibu yyako utaletewa papo kwa hapo.

Vipi kuhusu kujua asilimia ya bei ya punguzo uliyoona katika duka maarufu la nguo Mlimani City? Pia ni rahisi, andika asilimia ya bei ya punguzo kisha alama ya nyota(zidisha) kwa bei halisi na serach itakukomboa mara dufu.

Japo huduma hii si kubwa na ya kuzungumzia sana katika mfumo wa iOS 9, lakini ni muhimu na unahitajika sana. Badala ya kupanda na kushuka kwa bei za fedha kwenye Safari au Chromo, sasa kwa urahisi mkubwa unaweza kuangalia kwa kutumia ‘search’ katika simu yako. Kwa hesabu ngumu, unaweza kutumia Kikokotoo katika simu yako, lakini kwa hesabu rahisi na za haraka, serach ni mkombozi wa muda wako.
IOS 9 Ina vitu vipya vingi na vya kuvutia. Kama umekwisha uweka na kuutumia katika simu yako, tujulishe katika maoni yako apa chini ni vitu gani vipya vinakuvutia zaidi katika mfumo huu mpya, na vipi vinakukera.
No Comment! Be the first one.