Iwapo una Faili (file) ama Folda (folder) kwenye kompyuta yako na ungependa kulifanya lisionekane kwa wengine, unaweza kuficha Faili na Folda ili wengine wasiweze kuzifikia kwa urahisi.
Kwa bahati nzuri ni kwamba kwenye kompyuta za Windows hukuruhusu kuficha kila aina ya vitu kwa kutumia programu ambazo ziko ndani ya kompyuta yako (built-in tools) kama File Explorer ama unaweza kutumia njia ya Command kwenye programu za Command Prompt ama PowerShell.
- Jinsi ya kuficha Faili (File) na Folda (Folder) katika Windows 10 kwa kutumia File Explorer.
Kama unatumia Windows 10, Fungua File Explorer, kisha nenda mpaka kwenye file unalotaka kuficha. katika mfano huu nitatumia File ambalo limehifadhiwa kwenye Desktop ya kompyuta.
File Explorer mara nyingi inapatikana kwenye Taskbar, chini ya kioo cha kompyuta yako kwenye msitari unaoonyesha icons mbalimbali. Ukifungua File Explorer utaona vitu mbali mbali kama “This PC” na faili zingine kama Downloads, Documents, Pictures n.k
Right Click kwenye File unalotaka kuficha, utaona menu kisha bofya kwenye “Properties”
Ukiwa kwenye Properties, angalia na ufungue sehemu ya General, kisha nenda na ubofye kwenye kitufe kinachoonyesha “Hidden” na ukimaliza bofya kwenye “OK”
Ukibofya OK itakupeleka kwenye sehemu ya “Confirm Attribute Changes.” itakuuliza kama mabadiliko haya yafanyike kwenye Folda (Folder) hilo pekee au Folda hilo na vitu vyote vilivyomo ndani yake (sub folder), chagua sehemu unayotaka kisha bofya OK
Hapo utakuwa tayari umemaliza kuficha Faili (file) au Folda (Folder), Baada ya hapo rudi kwenye File explorer sehemu linakopatikana file unalotaka kuficha, bofya sehemu imeandikwa “view” inapatikana juu kwenye task bar, kisha nenda kwenye sehemu imeendikwa “Hidden items” kama imewekwa tick basi itoe hiyo tick na hilo file litafichwa.
Ukitaka kuangalia hilo faili au Folda lililofichwa, Fungua “File explorer” nenda kwenye sehemu faili lilipokuwa awali, bofya kwenye “view” kisha nenda kwenye “Hidden items” na uruhusu (tick) hapo utaona file ama folder lililofichwa pia linakuwa na rangi ya kijivu ili kutofautisha na mengine.
Kwenye Windows 11 kuna mabadiliko kidogo kwenye upande wa File explorer ukibofya sehemu ya “view” itakupa machaguo mengi, chagua sehemu imeandikwa “show” kisha nenda kwenye “Hidden items” hapo utaona faili na Folda zilizofichwa.
No Comment! Be the first one.