Ukiwa na mfumo wa ulinzi wa kamera (CCTV) kwa mfano na unataka kuziangalia kamera zako kwenye simu yako ya mkononi basi ni lazima kufungua port za mtandao wako kwanza, siyo kwa CCTV bali zipo nyakati kadhaa ambazo mtu kwa namna moja au nyingine huitaji kufungua port za mtandao wake ili aliye nje ya mtandao huo aweze kupata nafasi ya kuingia ndani ya mtandao husika.
Kwa lugha nyepesi kufungua port za ruta yako ni kuruhusu mtu au programu ambayo haiko katika mtandao wako kuwasiliana na mtandao wako kupitia port husika.
Kama kwa namna moja ama nyingine unataka ku-kipata kitu kilicho katika mtandao wako na wewe upo nje ya mtandao huo basi unahitaji kufungua port fulani ambayo ndio utaitumia kuingia katika mtandao wako, kwa mfano unataka ku-access mfumo wako wa CCTV popote ulipo, ama kama unataka kuchezaa baadhi ya michezo katika mtandao basi ni lazima ufungue port za mtandao wako
Angalizo. Lazima ijulikane kabla haujafanya lolote katika nitakayouyasema hakikisha unapata kibali kwa network administrator ama mtu mwenye mamlaka iwapo wewe hauna hayo madaraka maana kufanya hivi kunaweza kuvunja sheria za mmiliki wa mtandao huo.
Unapofungua port katika mtandao wako unaruhusu mtu/waty kutoka nje ya mtandao wako kuweza kuingia ndani ya mtandao wako hivyo inakupasa kuwa makini na kuhakikisha umechukua tahadhari zote za muhimu.
Baada ya kuyasema hayo sasa hebu tuangalie hatua za kufuata ili kufungua port za mtandao wako;
-
Kujua Anuani ya IP ya Ruta Yako.
Lazima ujue anuani ya IP ya ruta yako, hii itakuwezesha kuufikia ukurasa wa kufanyia mabadiriko ya mipangilio ya ruta yako.
-kama unatumia windows fungua sehemu ya kuandika komandi kwa kuandika “cmd” (bila alama za kufunga na kufungua semi) katika sehemu ya kutafuta katika menyu halafu ingiza komandi hii “ipconfig”(bila alama za kufunga na kufungua semi)
-anuani ya IP ya ruta hapa huoneshwa kama default gateway
Kama unatumia Mac; fungua terminal na kisha ingiza komand ya “netstat-nr”
Na kwa wale wanaotumia Linux basi fungua terminal na ingiza komand ya “route”
-
Inakili anuani ya IP tuliyo ipata hatua iliyopita na kisha ibandike katika browser yako na uifungue
-
Baada ya kuingiza anuani ya IP ya ruta yako na kufungua ukurasa utaona ukurasa wa kuingilia ambapo huu itategemea na ruta gani hasa unaitumia angalia hapa chini hizi ni kurasa za kuingilia kwa baadhi ya ruta.
-
Ni lazima utaombwa kuingiza nywila na jina la mtumiaji, kama haufahamu taarifa za router yako hizi hapa chini ni taarifa ya router zinazotumika zaidi
Kama ruta yako ni Linksys basi “admin” ni jina la mtumiaji na pia ni nywila
Kama ruta yako ni Netgear basi “admin” ni jina la mtumiaji wakati nywila ni “password”
Kama ruta yako ni tofauti na hizo zilizotajwa basi jaribu kutojaza kitu katika sehemu ya jina la mtumiaji na ile sehemu ya nywila andika “admin”
Kama haujui nywila na jina la mtumiaji vya ruta yako na njia zilizotajwa hapo juu hazija saidia basi fungua katika mtandao wa RouterPasswords.com ambapo utaingiza aina na namba ya ruta yako kupata nywila yake.
Lakini pia ikiwa uliweka nywila yako na umeisahau basi unaweza kuiupyisha ruta yako iwe na mipangilio ya kiwandani kwa kubonyeza kitufe cha kuiupyisha
-
Baada ya kuingiza nywila yako sasa utakua katika ukurasa wa kufanya mabadiliko ya ruta, tafuta sehemu ya kufungulia port. Muonekano hutofautiana saana inategemea na ruta unayotumia
Kila mtengenezaji anatumia maneno yake ila kufungua port kunaweza kupatikana katika menyu moja wapo wa hizi
PORT FORWARDING, APPLICATIONS, GAMING and(or) VIRTUAL SERVER
Kama hakuna neno linalofanana na yaliyo hapo juu basi tafuta ADVANCE SETTINGS na ukiingia ndani ya hiyo utakutana na neno PORTFORWARDING
- Utakapoingia katika “portforwarding” utakutana na list ya programu ambazo kwa kawaida huitaji kufungua port kwa hiyo unachotakiwa kufanya ni kujaza katika fomu taarifa za kifaa chako na kisha hakikisha umeiwezesha kufanya kazi (kwa kuwekea alama ya tiki) na baada ya hapo hifadhi mabadiliko yako
- Iwapo program unayotaka kuifungulia ports haipo katika mtiriliko uliopo basi inabidi utengeneze mpya kwa kujaza
- Jina la huduma unayotaka kufanya
- Jaza aina ya huduma unayotaka kutumia mfano TCP UDP ama Both
- Jaza port unazotaka zifunguliwe kwa huduma yako
- Jaza ip adress ya kifaa ambacho kinaendesha programu unayotaka ifunguliwe
No Comment! Be the first one.