Je ungependa kufuta akaunti yako ya Facebook? Kama unatumia mtandao wa kijamii wa Facebook na umechoka kuutumia mtandao huo au unataka ufute taarifa zako za huko na kuanza upya basi unaweza kufanya hivyo kwa kufuata hatua zifuatazo:
- Ingia kwenye menyu yako ya Facebook iliyopo juu kwenye kona ya kulia.
- Ukiwa kwenye hiyo menyu shuka chini mpaka uone sehemu imeandikwa Settings & privacy.
- Baada ya hapo ingia kwenye sehemu iliyoandikwa Settings.
- Ndani ya settings ingia kwenye sehemu ya kwanza ambayo itakuwa imeandikwa Personal and account information.
- Shuka mpaka kwenye chaguo la mwisho lililoandikwa Account ownership and control.
- Ukiwa humo utaona sehemu iliyoandikwa Deactivation and deletion, chagua hii
- Baada ya hapo utaulizwa kama unataka kuizima account yako ya Facebook kwa muda au unataka kuifuta kabisa account yako, Hapa utachagua inayokufaa kisha utatakiwa kuingiza nywila yako.
Angalizo: Akaunti ya Facebook hufungwa siku 30 baada ya kutuma maombi ya account yako kufungwa.
No Comment! Be the first one.