Utaalamu huu ambao TeknoKona imekuandalia leo, hautajalisha kama unabadilisha simu yako kwenda kwenye simu nyingine ambayo ni kampuni moja kama ile uliokuwa unatumia mara ya kwanza au la…
Hii ikiwa na maana kuwa utakuwa na uhuru wa kubadilisha kwenda katika mfumo wa simu wowote unaoutaka kwa mfano unaweza ukatoka Android ukaenda iOS au ukatoka iOS ukaja Android. Hapo sasa usiwe na uwogo juu ya taarifa zako, kwamba utazipata vipi
Acha TeknoKona Ikujuze Njia Hizo Sasa
Android Kwenda Android
Kama unataka hamisha taarifa zako kutoka Android kwenda Android ni rahisi sana. Asante kwa huduma za uhifadhi wa mtandao (Cloud Service) kutoka Google. Hii inafanya jambo la kuhamisha taarifa liwe rahisi sana hasa kama unatumia programu endeshaji mpya, Android 5.0 (lollipop)
Japokuwa wazalishaji wakubwa wa simu za Android huwa wanakuwa na njia zao za kuhamisha vitu katika vifaa vyao kwa mfano Samsung wana Smart Switch na pia Motorola wana Migrate, zote hizi zikiwa na lengo moja
Programu endeshaji kwa upande mwingine ina vipengele viwili vipya ambavyo ukivitumia unaweza ukahamisha taarifa zako hizo bila shida. Vipengele hivyo ni Tap & Go na ‘Get Your Apps & Data’
– Tap & Go
Kipengele hichi kinatemea teknolojia ya NFC ili kukamilisha uhamishaji wa taarifa zako. Mara tuu ukishachakua Tap & Go wakati ukiwa unaaza kutumia simu yako kwa mara ya kwanza itakubidi uchukue simu yako ya zamani ya Android na kisha uwashe NFC
Washa kwenye simu zote mbili, hapo taarifa zitaanza kujihamisha baada ya wewe kubofya ‘Okay’. Meseji yenye ujumbe itajitokeza katika simu mpya kama taarifa zikimalizika kujituma
– Get Your Apps & Data
Kama simu yako ya zamani haina teknolojia ya NFC achana na Tap & Go na kisha tumia njia hii. Kama ukiwa unatumia barua pepe moja katika akaunti yako ya Google hii itakuwezesha kupata taarifa zako katika simu yako mpya. Njia hii itawezekana kama ulifanya BackUp kwa kutumia simu yako ya zamani. Kabla ya kuendelea na njia hii inakubidi uwe na uhakika kama simu yako ilikuwa ukihifadhi mafaili yako katika hifadhi ya kimtandao ya Google
Angalia ili kupata uhakika hapa Settings > Personal > Backup & reset. Na kisha hakikisha ‘Back Up My Data’ imewashwa.
Ukishapata uhakika kwamba una hifadhi ya taarifa zako muhimu (Back Up) basi chagua ‘Get Your Apps & Data’ katika simu yako mpya na itakupa list nzima ya App ambazo zipo katika simu yako ya zamani. Kuna baadhi ya App zinaweza zisitokee katika listi hiyo ila sio mbaya kwani unaweza ukazishusha tena katika soko la Google Play Store
Ili kupata Picha, Mafaili n.k. huna budi kutumia huduma za Google kama vile Google Drive au ile maarufu ya kuhifadhi pich aijulikanayo kama Google Photos
iPhone Kwenda iPhone
kama umechukua simu mpya ya iOS kama vile iPhone 6 au hata iPhone 6 Plus njia ya uhamishaji wa taarifa zako ni rahisi sana, asante kwa iCloud!
Kabla huajaanza kuhamisha taarifa katika simu yako mpya hakikisha kama simu yako ya zamani ilikuwa inahifadhi vitu katika iCloud. Kuangalia nenda katika Settings > iCloud > Backup. Kama ulikuwa hufanyi ‘Back Up’ huna budi kufanya kwanza kabla ya kuendelea kwa kuchagua ‘Back Up Now’
Sasa unaweza ukaanza kuihudumia simu yako mpya. Baada ya kuingiza taarifa zako za akaunti yako ya iCloud itakuambia uchague kati ya ‘Restore From Back Up’ au ‘Set Up The Phone As New’. Chagua chaguo la kwanza (Restore From Back Up), na ukifanya hivyo utaanza kupokea taarifa zako!
Android Kwenda iPhone
Unaweza ukapata taarifa zaidi katika ukurasa wa Apple ukiwa unaelezea ‘kubadilisha na kwenda katika iPhone’ (Switch to iPhone) na kisha unaweza amua kushusha app hiyo kutoka katika soko la Google Play.
Ukishamaliza kuiweka App ya ‘Move to iOS’ katika simu yako unaweza ukaanza kuhamisha taarifa zako za kalenda, namba za simu, akaunti za barua pepe, meseji, picha, video n.k. yote haya yatawezekanana kama kifaa chako cha iOS kikiwa kipya kabisa (yaani ndio unaanza kukitumia)
iPhone Kwenda Android
Hapa hakuna App ambayo inafanya kila kitu yaani kuhamisha kila kitu yenyewe ila mtu unaweza ukatumia App kama vile Google Drive ili kuhamisha baadhi ya taarifa. Kama hutumii Google Drive unaweza ukatafuta App zingine ambazo zinaruhusu huduma ya uhifadhi wa kimtandao (Cloud Service)