Mara nyingi watu tunakua na mitandao mingi ambayo mara nyingine huwa inafanya kazi sawa kwa mfano unaweza ukawa unahifadhi namba kwa kutumia Android huku unahifadhi zingine kupitia iOS.
Kama unatumia huduma ya Outlook na pia ukawa unatumia pia ya Google kwa upande wa kalenda kuna namna unaweza ukaunganisha kalenda hizo mbili na kuanza kuzitumia katika eneo moja (Google).
Kama usipounganisha na kuonekana katika sehemu moja basi utakua na ulazima wa kuweza kutumia huduma moja moja kwa wati tofauti ili kupata huduma hizo
Hii Hapa Ni Njia Ya Kuunganisha Huduma Hizo
- Kwa kutumia kompyuta ingia katika tovuti ya Outlook na kisha ingia katika akaunti ya Microsoft.
- Nenda katika eneo la ‘Calendar’ na kisha ingia katika eneo la ‘Settings’
- Chagua eneo la ‘Shared Calendar’ kuchagua kalenda yako ya kimtandao.
- Chagua eneo la ‘Can View All Details’ katika eneo la ruhusa na kisha chagua neno ‘Publish’ ili kuruhusu.
- Utaona kuna link za GTML na ICAL na kisha ‘Copy’ link hizo.
- Nenda katika mtandao wa Google na ingia katika Google Calendar katika mtandao.
- Gusa katika alama ya + katika eneo la My Calendar/Other Calendars na kisha chagua from URL
- Ingiza (PASTE) ile link ya ICS ili kuoneza ile kalenda kutoka Outlook.
Mpaka hapo utakua ushakua umeweza kufaniisha hilo. Kingine ni kwamba usishagae kama kalenda hizo kutoka Outlook itakua kama bado haijaingia katika kalenda ya Google huna budi kusubiri kidogo.
Ningependa kusikia kutoka hapo, je wewe unatumia kalenda zote mbili na ungependa kalenda zote zipatikane eneo moja? Niandikie hapo chini katika eneo la comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.