Kuna watu wengi wanapata shida sana juu ya kulinda taarifa juu ya akaunti zao za Facebook. Kubwa kuliko yote ni nani aone vitu wanavyoposti au hata kuzuia watu kuwa ‘tag’ watu wengine bila hiari yao katika picha ambazo haziwahusu. Ndio kuna mambo mengi yanakera! lakini kuna njia za kuondokana na hayo mambo.
Je una wasi wasi kuna watu wanapenda kukuchunguza chunguza katika mtandao wa facebook?, Teknokona inakujuza maujanja leo juu ya jinsi gani unavyoweza kulinda taarifa zako (Picha, Picha Ya Profaili, Posti, Ujumbe na Marafiki).
- Kwanza kabisa inabidi ufungue akaunti yako ya facebook na kwenda katika eneo la ‘Settings‘ kisha chagua ‘Privacy‘. Sasa hapo katika upande wa kulia (kama unatumia Kompyuta) unaweza ukachagua nani anaweza kuona taarifa zako
Katika eneo hilo la privacy lina vitu vitatu yaani Who can see my stuff?, Who can contact me? na Who can look me up? (Nani anaweza ona mmambo yangu?, Nani anaweza wasiliana nami? na Nani anaweza nitafuta). Kila kipengele kina maelezo yake juu ya kubadilisha na kuweka machaguo sahihi mtu anayoyataka kwa mfano katika kipengele cha Who can look me up? mtu anaweza amua kuweka chaguo la kutafutwa na kila mtu kwa kutumia barua pepe yake anayotumia
- Ukishamalizana na kipengele cha ‘Privacy‘ sasa bofya kwenye kipengele cha Timeline and Tagging. Utaona vitu mbali mbali vya kubadilisha kulingana na kitu gani unataka.
Vipengele ukavyokutana navyo ni Who can add things to my timeline?, Who can see things on my timeline? Na How can I manage tags people add and tagging suggestions? (Nani Anaweza ongeza vitu katika ukurasa wangu?, Nani anaweza ona vitu katika ukurasa wangu Na jinsi gani naweza kuendesha mfumo mzima wa ku ‘tag’). Kwa mfano katika kipengele cha Who can add things to my timeline? unaweza chagua marafiki zako waweze ongeza vitu katika ukurasa wako
Baada ya yote hayo nenda katika kipengele cha Followers (Wanaokufuata) na chagua Who can Follow me? (Nani wakuni fuata) kuliangana na mapendekezo yako unaweza chagua kutoka kwa Marafiki na kwenda kwa kila Mtu
- Baada ya kukamilisha yote hayo basi ngoja Tufiche taarifa zako binafsi
- Nenda katika Sehemu Profile katika Facebook na kisha chagua About.
- Bofya katika ‘Update Info’ na uanze fanya maboresho juu ya nani aone taarifa zako za muhimu. Mfano katika kipengele cha ‘Contact and Basic Info’ siku, tarehe na mwaka wa kuzaliwa unaweza bofya kwenye ki alama cha dunia kile na kuchagua nani anaweza ona taarifa hiyo. Unaweza fanya marekebisho mengi hapo yanayohusiana na Profile lako kwa ujumla.
Kwa kujua hayo mambo (vipengele) manne ya muhimu basi unaweza kuwa na uhakika wa taarifa zako za mtandao wa facebook. Kuna wengine wanakosa amani na uhuru katika mtandao huu, hilo litakua limefika kikomo sasa. Kwa mtindo huu hutaoata usumbufu wa ajabu ajabu kwa watu usiofahamiana nao.
Wazo lako ni muhimu, ningependa kusikia kutoka kwako pia tafadhali ungana nasi kupitia kurasa zetu za Facebook ,Twitter, Na Instagram
No Comment! Be the first one.