Hili sio jambo geni kwa watumiaji wa Android lakini katika iPhone limechelewa kufikia. Kwa sasa kwa uwezo wa Face ID au hata ile njia ya passcode hili linawezekana.
Watumiaji wa iPhone nao hawajasahaulika na hili sio gumu sana kulifanya. Mara kwa mara simu zetu zinashikwa na watu wengi na vile vile huwa tunatamani watu wasiweze kuingia katika baadhi ya App.
Suluhisho inakua ni uwezo wa kuzifunga App hizo kwa kutumia Passcode au Face ID ambayo tayri ipo katika iPhone yako.
Ili kuhakikisha kwamba unawezesha kulifanya hili ni lazima uwe unatumia toleo la iOS 16.4 na kuendelea maana chini ya hapo halitawezekana kiurahisi.
Kingine ni kwamba kwa kutumia njia hii ni kwamba App hiyo kama ikitokea ikifunguliwa –labda na mtu mwingine –moja kwa moja itaji’lock.
Uli uweze kutumia App hiyo inamaana lazima utumie passcode au utumie face ID katika iphone na ili kuliwezesha hilo itakubidi utumie njia ifuatayo.
Katika iPhone yako fungua App ya Shortcuts
Ingia katika eneo ambalo limeandikwa Automation katika upande wa chini kabisa wa kioo
Ukishaingia nenda katika alama ya + ambayo ipo upande wa juu kulia kabisa katika App hiyo na kisha ingia katika Create Personal Automation
Shuka chini na kisha chagua eneo la App na kisha chagua App ambayo unataka kui’lock
Katika orodha ya App itakayo tokea chagua App ambayo unataka kui’lock na kisha chagua neno Done.
Ingia katika neno Next ambalo liko katika upande wa juu kabisa kulia katika uso wa kioo cha simu yako na kisha ingia katika neno Add Action ambalo lina maandishi ya bluu.
Katika eneo la kutafuta (search) andika neno ‘lock screen’ na kisha likitokea lichague kwa kuingia katika eneo la Next
Funga chaguo la Ask Before Running
Katika window mpya ambayo itatokea chagua neno Don’t Ask alaf chagua neno Done.
Mpaka hapo utakua umefanikisha hilo na hali hii itaanza kufanya kazi mara baada tuu ukiwa unafungua App husika.
Unaweza kufanya hivi kwa App zote zile unazozitaka, zote utatumia njia hii hii tuu.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment? Je hii umeipokeaje? Je ushawahi kukutana na njia hii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.