Mara nyingi kompyuta zetu zinakuwa taratibu (slow) kwenye ufanyaji kazi ( ukifungua programu au kitu chochote) inachukua mda mrefu kufungua au kufanya kazi husika. Hii imekuwa ni kero kwa wengi na pia inasababisha watu wengi kushindwa kufanya au kumaliza kazi kwa wakati.
Kuna njia kadhaa za kufanya ili kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la kompyuta kufanya kazi taratibu na hivyo kuifanya kompyuta yako kufanya kazi haraka.
NJIA 1: ZIMA PROGRAMU ZISIZOTAKIWA (DISABLE UNWANTED START UP PROGRAM)
Unatakiwa kuzima au kuzuia programu zote ambazo huzitumii lakini bado zimewashwa ( programs running on background) hizi huendelea kuchakatwa na kompyuta hivyo kufanya kompyuta yako kuwa taratibu kwenye kazi zake sababu programu nyingi zinatumika kwa wakati mmoja.
NJIA ZA KUFUATA
Right click kwenye start menu > nenda kwenye “Task manager” > bofya kwenye “Startup option” (hapa utaona programs zote zinazotumika kwenye kompyuta (run background)
Programu hizi hutumia sehemu za kuhifadhi kumbukumbi (memory) hivyo husababisha kompyuta kuwa taratibu kuliko kawaida.
Jinsi ya kuzima programu.
bofya kwenye program unayotaka kuzima > nenda kwenye “Disable”
NJIA 2: FUTA FAILI ZILIZOTUNZWA KWA MDA (DELETE UNNECESSARY TEMPORARY FILES)
NJIA ZA KUFUATA:
Right click kwenye start menu > bofya sehemu imeendikwa “Run” > kwenye kiboksi andika %temp% > kisha bofya “ok”
baada ya hapo kompyuta itafungua faili myingi, zifute zote hizo faili.
ukimaliza hiyo hatua
right click kwenye start menu > fungua “Run” > andika “temp” > bofya kwenye “continue” > chagua faili zote na uzifute.
NJIA 3: SAFISHA SEHEMU YA KUMBUKUMBU (CLEAN UP MEMORY)
Nenda kwenye “This Pc” ya kompyuta > right click kwenye drive ( C: ) > bofya kwenye properties > nenda kwenye sehemu ya “General” > bofya “Disk Cleanup” kompyuta itachunguza (scan) faili na endapo ikimaliza bofya kwenye “Cleanup system files” > bofya OK kisha bofya kwenye “Delete files”
NJIA 4: ONDOA PROGRAMU USIZOZIHITAJI (UNSTALL UNWANTED PROGRAMS)
Right click kwenye start menu > chagua “settings” >kisha “Apps” > bofya kwenye “Apps and features” > Chagua Program ya kutoa > bofya “unstall”
NJIA 5: TUMIA ANTI-VIRUS
Tatizo jingine ambalo hufanya kompyuta kuwa taratibu ni uwepo wa wadudu (viruses) kwenye kompuya husika, hivyo unaweza kufanya uchunguzi (scanning) ili kubaini kama kompyuta ina wadudu au la.
Unaweza kutumia antivirus uliyoweka kwenye kompyuta au aidha kompyuta zinazotumia Windows huja na anti-virus inayoitwa Windows defender.
Jinsi ya kuchunguza wadudu kwenye kompyuta (viruses scanning)
Right click kwenye start menu > nenda kwenye settings > bofya “Update & security” > nenda kwenye Windows security > bofya kwenye “Virus and Threat protection” > ukifungua hapo utaona sehemu ya “Scan options” unaweza kuchagua Full scan > utasubiri kompyuta imalize ku-scan kisha utafata utaratibu namna kuondoa wadudu (viruses) kama wakipatikana.
Yafaa kompyuta iwe na kasi nzuri pindi uitumiapo, lakini pia ni muhimu kuelewa uwezo wa kompyuta yako na aina ya kazi unapaswa kuzifanya, usiibebeshe mzigo mkubwa kompyuta ingali uwezo wake ni mdogo, hizo njia hapo juu zitakusaidia kuifanya kompyuta yako kuwa na kasi katika ufanyaji kazi wake.
Unaweza pia kusoma makala zetu zingine hapa.
No Comment! Be the first one.