WhatsApp ni moja kati ya mitandao ya kijamii yenye umaarufu mkubwa sana bila kusahau ubora wake unaifanya kila siku kuaminika kama njia ya mawasiliano.
Ndani ya mtandao huo wa WhatsApp huwa watu wanatumiana vitu mbalimbali kama vile miziki, video na mafaili mengine ambayo kwa namna moja au nyingine inasababisha ujazo uhifadhi wa mtandao huo kujaa.

Ukaichana na kujaa tuu kwa mtandao huo kingine ni kwamba inapelekea mpaka kifaa unachotumia –simu– kujaa katika ujazo uhifadhi wake.
Mara zote ili kujihakikishia una ujazo uhifadhi wa kutosha katika kifaa chochote ni kuhakikisha kuwa unapunguza vitu ambavyo havina ulazima au vitu hivyo huvitumii mara kwa mara.
Kama WhatsApp itakua imejaa ujazo uhifadhi ya kifaa chako –simu– kitakua kimejaa ujazo uhifadhi kuna muda unaweza ukawa unafungua App hiyo lakini bado ikagoma kufunguka na kukuamuru upunguze vitu kwanza.
Mara nyingi hali hiyo ikifika hata meseji mpya katika kifaa hicho hazitakua zinaingia tena. Kama jambo hili limefikia kuna kitu unaweza fanya na mambo yakawa sawa.
Pengine sio lazima hata jambo hili kufikia, unaweza ukatumia njia ifuatayo katika kuhakikisha kwamba adha hii haikupati.
Ndani ya mtandao huu, unaweza ukaingia katika eneo la “Storage and Data” na ukishangia hapo utaweza kuona mafaili yote ambayo umeshawahi kutumiwa katika mtandao huo na yana ukubwa wa kiasi gani.
Kingine kizuri ni kwamba mafaili hayo yatakua yametengwa katika mfumo ambao utakuonyesha kua ni mafaili gani ambayo yamechukua nafasi kubwa na yale ambayo yamechukua nafasi ndogo zaidi.
Hapo unaweza ukaanza kuchagua mafaili ambayo unataka kuyafuta kwa lengo la kuhakikisha unaongeza ujazo uhifadhi wako.
kingine cha msingi kama kuna maongezi (chats) ambayo sio ya muhimu kubaki katika App hiyo basi nayo ukiyafuta kwa namna moja au nyingine yanasaidia katika kuhakikisha kuwa ujazo uhifadhi unaongezeka.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je umeshawahi kufikwa na adha hii ya ujazo uhifadhi kujaa katika simu yako mpaka App ya WhatsApp kushindwa kufunguka? njia gani ulikua unatumia ili kuhakikisha kua App hiyo inafunguka vizuri?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.