Katika hali ya kawaida kabisa inaweza kutokea wakati unaperuzi mtandaoni kupitia kompyuta ama kwa kudhamiria au bahati mbaya inatokea unafunga kurasa kivinjari kitendo ambacho kitasababisha kupoteza uwezo wa kuzifikia kiurahisi kurasa husika.
Wazo la kutoka somo kuhusu makala husika ni kitu ambacho kimeshanitokea mara nyingi tuu jambo ambalo lilinifanya kufedheka kwa kiasi fulani kutokana na kwamba nakuwa nimepoteza mbinu ya kuperuzi kwenye kurasa nyingi kiurahisi kabisa kupitia kivinjari. Hivi karibuni nilivyojikuta kwamba nimefunga kwa bahati mbaya kivinjari cha Google Chrome nikasema safari hii lazima nizirudishe bila kuteseka.
Rudisha kurasa ulizozifunga kwenye Windows/MacOS
Katika hali ya kawaida tuu unapopatwa na tatizo ndio akili inafikiri zaidi ili kuweza kutatua changamoto iliyokufika. Sasa kwa wale ambao tunatumia kompyuta zenye programu endeshi ya Windows ikitokea tu umefunga kivinjari chako kitendo ambacho kitasababisha kupoteza kurasa ambazo ulikuwa tayari umeshazifungua basi mara baada ya kufungua Google Chrome, Mozila, Opera Mini bofya CTRL+SHIFT+T ili kuzirusisha kurasa ulizokuwa umezifunga. Kwa wale wanaotumia kompyuta za Apple ama kwa lugha rahisi MacOS basi ukibonyeza Command(Cmd)+Shift+T kurasa zitarejea kama zilivyokuwa hapo awali.
Kwa wale ambao tunapenda kwenda hatua kwa hatua basi ukishafungua kivinjari cha kwenye kompyuta yako angalia upande wa kulia juu kwenye zile nukta tatu zilizofuatana bofya kisha nenda moja kwa moja palipoandikwa History>>Reopen Closed tabs (Ctlr+Shift+T) kisha bonyeza na hapo zile ambazo zilitoweka mara baada ya kufunga Chrome, Mozilla Firefox zitarudi.
Kimsingi kuna raha ya kutumia kicharazio kuweza kufanya mambo mengi yanayohusisha matumizi ya kompyuta ingawa si vibaya pia ukiamua kutumia njia ndefu kufanikisha kile ambacho unahitaji.
Vyanzo: Free Code Camp, Business Insider
No Comment! Be the first one.