Je unafahamu jinsi ya kuscan kompyuta yako na faida zake? Kompyuta zinazokuja na Windows 10 au 11 ndani yake zinakuja na program ya Windows Defender (built-in Antivirus) ambayo hufanya kazi muda wote ( Run on background), hii inasaidia kupambana na wadudu (viruses) ambao husababisha uharibifu kwenye utendaji kazi wa programu endeshaji na programu zingine.
Hakikisha Windows defender inafanya kazi mda wote na umeweka masahihisho ya mara kwa mara (Automatic updates)
Unaweza kuchanganua (scan) kompyuta yako kama kuna wadudu (viruses) na ukasafisha (clean-up) kuondoa hao wadudu.
Virusi vya kompyuta ni programu kama programu nyingine lakini zlizotengenezwa kwa lengo la kuingilia au kuharibu utendaji kazi au mfumo wa kompyuta. Fahamu zaidi kuhusu virusi hapa ->Mambo 11 Yakushangaza Kuhusu Virusi vya Kompyuta
UNAWEZAJE KUCHANGANUA (SCAN) KOMPYUTA YAKO?
Fungua Windows Security
Hatua za kufuata
a) Fungua windows settings ( start button + settings)
b) Bofya kwenye “updates and security“
Hapa utaona kama kuna masahihisho yoyote (windows updates) au kama kuna windows defender updates utaziona.
c) Chagua Windows security kisha bofya sehemu ya “open windows security“
d) Chagua “Virus and Threat protection” kwenye ukurasa wa “viruses and protection”
Hapa unaweza kuona changanuzi za nyuma (scan history) au chagua “protection history” kuona kama kuna changanuzi/scan zilizofanyika kipindi cha nyuma na kama wadudu/viruses walionekana.
Ukiwa bado upo kwenye ukurasa wa “Virus and Threat protection”
d) Bofya kwenye scan type, chagua “scan options” chagua kipengele cha “Windows Defender Offline scan” kisha bofya kwenye scan now.
Kwanini offline scan
Hii huchanganua/scan kwenye files ambazo haziwezi kufutwa (system files) endapo kompyuta inafanya kazi hii ni kwa sababu hufanya kazi kwenye hali ya nje ya mtandao (offline mode).
Unaweza pia kuchagua kipengele cha “Full scan” ambacho huchanganua/scan kwenye kila file kwenye kompyuta husika, inachukua muda kulingana na uwezo wa kompyuta.
Ni muhimu kufanya changanuzi/scan kwenye kompyuta yako mara kwa mara ili kuifanya kompyuta yako kuondoa wadudu/viruses na kuifanya kompyuta yako kufanya kazi vizuri. Ni muhimu pia kufanya masahihisho ya mfumo wa kompyuta yako (Software updates) kwa ajili ya ulinzi, usalama na ufanisi wa kazi.
No Comment! Be the first one.