Baada ya kuandika jinsi ya kushusha (kudownload) video kutoka facebook moja kwa moja kwa kutumia kompyuta muamko umekuwa ni mkubwa sana. Wengi wamepongeza makala hiyo na wakaomba namna ya kuweza kujua wataweza vipi kuzishusha video hizo wakiwa wanatumia vifaa vyao vya android.
Kama kawaida ya TeknoKona, timu imepitia maombi hayo na kuja na makala hii. Kuwa na video katika kifaa chako ni kitu kizuri sana hasa ukiwa na zile za kuchekesha. Hebu fikiria kama kama kuna mtu kakuudhi au uko vibaya siku hiyo na ukaamua kuangalia baadhi ya video katika simu yako, hali yako itabadilika kidogo kutoka katika ubaya uliokua nao na kuelekea katika uzuri.
Katika zoezi hili kuna njia mbili
NJIA YA KWANZA
Kama umeingia facebook kwa kutumia kivinjari cha chrome katika kifaa chako
- fika katika video unayotaka kushusha na kisha ichezeshe. Inapoanza kucheza ibofye mda mrefu bila kuachia, kufanya hivyo litatokea chaguo la “Save video”
- Bofya “Save video” na itaanza moja kwa moja kushusha video hiyo.
- Video hizo unaweza kuzipata katika Gallary kwa urahisi kabisa, lakini kama usipoziona unaweza ukaingia katika File Manager na kuanza kuzitatafuta katika folder la video.
NJIA YA PILI
Kutokana na kwamba App ya facebook hairuhusu kudownload video moja kwa moja, ni lazima utumia App za nje ili kuweza kufanya hili. App ziko nyingi sana ambazo zinaweza mruhusu mtumiaji wa facebook akaweza shusha video mbalimbali katika mtandao huo wa facebook kinyemela.
Njia hii ya pili itakuwezesha kuweza kushusha video hizi kwa kutumia App kutoka katika soko la android (Google Playstore).
Jinsi Ya Kushusha Na Kutumia App Hii
- Ingia katika Google Play Store na Kisha Shusha App hii “MyVideo Downloader for Facebook” na kisha ifungue
- Ukishaifungua, ingia katika App hii kwa ku’log in’ katika akaunti yako ya facebook
- Bofya katika mishale mitatu (Menu) upande wa kushoto
- bofya katika eneo la My videos na yatatokea machaguo mengi kwa ajili yako
- Kama uli Like video hiyo bofya katika Liked videos.
- Itaonyesha video zote ulizozikubali, hapo unaweza bofya download ili kupakua video hizo
- Baada ya kushusha video hizo unaweza kuzipata katika simu yako kule katika eneo la Gallary.
Njia zote mbili ni rahisi sana. Pia kuna App nyingi sana zinazoweza kulifanikisha hili lakini Teknokona inashauri utumie hii (MyVideo Downloader for Facebook) kwani ni rahisi sana kutumia.
MUHIMU: Njia hizi zitaweza kufanya kazi kwa video zile ambazo zilipakiwa (upload) katika mtandao wa facebook moja kwa moja na si vinginevyo. Kwa mfano video zote ambazo zimewekwa kama link kutoka mitandao mingine kama youtube hazitakubalia
SOMA PIA: Jinsi Ya Kushusha (Kudownload) Video Kutoka Facebook Moja Kwa Moja
No Comment! Be the first one.