Tangia mtandao wa kijamii wa Facebook ulipoweka huduma/kipengele chake cha kuwawezesha watumiaji wake waweze kupakia na kuangalia video za aina mbalimbali kutoka katika mtadao huo imekua ni safi sana. Watu sasa hivi wakiwa katika mtadao huu hawategemei ujumbe na picha tuu.
Kumbuka unaweza kuona video katika mtandao huo wa Facebook na ukatokea kuipenda sana, sasa kuna njia ya kuipata video hiyo ukiwa katika kivinjari chako bila hata ya kuwa na App nyingine ya kufanya zoezi hili (kushusha)
Kwa kufuata njia zifuatazo utaweza kushusha video kutoka katika mtandao wa kijamii wa Facebook na kuzihifadhi katika kompyuta yako bila ya kuwa na App nyingine mbadala.
- Fungua mtandao wa facebook katika kivinjari (Google Chrome, Internet Explorer ndivyo tunavyopendekeza) na nenda mpka katika video unayoipendelea kuishusha
- Bofya katika video hiyo kwa lengo la kuifungua kwa ukubwa (full screen)
- Sasa katika sehemu ya kuandika tovuti inabidi ufanye mabadiliko kidogo kwa mfano kutoka https://www.facebook.com/video/xyz na kubadilisha kuwa https://m.facebook.com/video/xyz cha msingi hapa ni kwamba utaondoa www za mwanzo katika tovuti na utaweka herufi m (mwanzoni) na utabofya Enter.
Angalia Picha Kwa Kuelewa Zaidi
Mfumo wa simu wa Facebook ukiwa na hiyo video utatokea na kisha unaweza kubofya katika video hiyo ili ianze kucheza
Video ikishaanza kucheza unaweza uka ‘right click’ na kusha ukachagua Save video as… katika machaguo ambayo yatajitokeza.
Katika ukurasa(window) mpya ambayo itatokea unaweza chagua sehemu ya kuhifadhia video hiyo na unaweza hata kubadilisha jina la video hiyo (hapo utakuwa umeihifadhi video hiyo)
Video hiyo kutoka Facebook itaanza kujishusha na kujihifadhi katika kompyuta yako.
No Comment! Be the first one.