Watumiaji wa mtandao wa Google sasa wanaweza kushusha (Download) kumbukumbu za vitu mbalimbali walivyowahi vitafuta kupitia Google.com, na hii ni kulingana na maelezo yaliyotolewa katika mtandao wa kampuni hiyo.
“Hii inakuwezesha kupata taarifa zako mahali popote na wakati wowote unapozihitaji” – Google iliandika kuhusiana na huduma hii
Uwezo wa google kuwa na “search history” yaani historia ya vitu ulivyotafuta ulikuwepo toka zamani lakini hili la watumiaji kuweza kushusha data hizo umeanza January ambapo ndipo ilipo zinduliwa.
Taarifa hii mwanzo iliripotiwa Aprili 18 2015 na blog isiyorasmi/isiyotambulika ambayo iliitwa “Google Operating System” na pia karipoti haka kalipata umaarufu sana katika mtandao.
Jinsi Ya Kufanya Hivyo Fuata Hatua Hizi Nne
1. Nenda katika Google Web history yako. (Itakubidi u ‘Log in’ katika akaunti yako) – BOFYA -> https://history.google.com/history/
2. Click kialama kilichopo juu kwenye kona upande wa kulia na kisha click “download.”
3. Kuna box litatokea mabalo linasema “Please read this carefully, it’s not the usual yada yada.”
4. Utapata email ikiwa kama uthibitisho ndani yake kutakuwa na link ambayo inakupeleka moja kwa moja mpaka sehemu data zako zilipo. Data hizo zitakuwa katika google drive katika upande wa “Takeout folders” ambayo yanaweza kushushwa katika kompyuta
No Comment! Be the first one.