Watu wengi hufikiri simu haziwezi kupata wadudu (viruses) lakini ukweli ni kwamba simu inaweza kupata wadudu (viruses) kama ilivyo compyuta (computer), maana pia tunatumia simu zetu kufanyia kazi mbalimbali. wadudu (viruses) wapo wa aina nyingi na wana kazi mbalimbali.
Simu zote zina uwezo wa kupata wadudu (viruses) ila simu zinazotumia programu endeshi ya Android (Android smartphone) ndiyo zipo kwenye hatari kubwa ya kupata wadudu kulingana na mfumo wake wa uendeshaji wa simu ukilinganisha na simu zenye iOS (iPhone).
DALILI AMBAZO HUONYESHWA NA SIMU YAKO KAMA INA WADUDU (VIRUSES)
1: Matumizi makubwa na internet bundles
Mara nyingi unaweza ukaona internet bundle kwenye simu yako inatumika na kuisha kwa haraka, hii inaweza kuwa dalili kwamba viruses wanatumia internet bundles ya simu yako pasipo wewe kujua (run on background) au pengine wadudu hutumia internet ya simu yako kusafirisha taarifa kutoka kwenye simu yako kwenda sehemu nyingine. Na hii hutokea pale unapopakua (download) programu (Apps) ambazo/ambayo siyo salama au faili/file ambalo siyo salama, huambatana na wadudu ndani yake.
2. Programu (Apps) kutofanya kazi ipasavyo.
Mara nyingi unaweza kuona baadhi ya programu (apps) kwenye simu yako zinajifunga au pengine kutofanya kazi kabisa (App crashing), kama tatizo hilo likitokea mara kwa mara inaweza kuwa ni dalili ya simu kuingiliwa na wadudu.
3. Matangazo mengi kwenye simu yako (Adware pop-ups )
Siyo kila tangazo linalokuja kwenye simu yako ni wadudu, kuna matangazo mengine yanakuja kulingana na vitu unavyopenda kufaya mara kwa mara kwenye simu, ila ukiona matangazo mengi yanakuja juu ya simu yako hata kama hujaingia mtandaoni ni dalili mojawapo ya simu yako kuingiliwa na wadudu.
4. Programu (Apps) zisizoeleweka
Ukiona programu/apps kwenye simu yako huijui na wala hujawahi kuipakua (download) kuwa makini sana mara nyingi huwa ni programu ambazo si salama (fake apps) na zipo kwenye simu kwa lengo la kukusanya taarifa zako, na nyingi zinakuja endapo unapakua (download) kitu kutoka sehemu ambayo siyo salama.
5. Battery kuisha kwa haraka na simu kupata joto (overheating)
Mara nyingi unaweza ukaona simu yako inaisha betri/battery kwa haraka na inapata joto sana hii ni kwasababu wadudu/viruses waliopo kwenye simu wanatumia nguvu nyingi kufanya kazi hivyo hujikuta wanatumia betri kwa kiwango kikubwa kuliko matumizi ya kawaida na kupelekea simu kupata joto sana, ukiona dalili ya simu yako kuishiwa betri kwa haraka isivyo kawaida hiyo inaeza kuwa mojawapo ya dalili kuwa simu yako imepata wadudu.
JINSI YA KUTOA/KUJILINDA NA VIRUSES
1: Tumia programu za antivirus kwenye simu yako, hii itasaidia kujikinga na wadudu/viruses wanaoweza kuingia kwenye simu na kuharibu/kuiba taarifa zako.
2: Sasisha mfumo wa uendeshaji wa simu yako (Update operating system (OS)), mara kwa mara kila wanapotoa sasisho(updates), mara nyingi hizi updates zinasaidia kuziba mianya ambayo huenda ilikua ni chanzo cha wadudu kuingia kwenye simu.
3: Usibofye (click), kupakua (download) wala kufungua kitu chochote ambacho hukijui na kama hakitoki sehemu rasmi na salama, mara nyingi viruses huingia kupita viambatanisho (attachments) ambazo unapakua/download.
4: Ondoa Programu hatarishi (Unstall malicious apps)
Unaweza kutoa programu zote ambazo apps zinaleta uharibifu kwenye simu, njia nzuri ni kutumia SAFE MODE. Kwenye safe mode ya simu unazuia programu/apps zote kufanya kazi pasipo kujua (on background) na unaweza kutambua kama kuna kitu cha tofauti kwenye simu yako.
Restart/Reboot simu yako, kwa haraka bofya ( power button + volume down) uweze ku-restart kwenye safe mode.
Baada ya kurestart kwenye safe mode bofya “settings” >> manage apps/apps & notifications >> Downloaded or installed apps >> angalia apps usizozihitaji kisha zitoe.
Wadudu wakiingia wakiingia kwenye simu huweza kusababisha madhara mengi ikiwemo kuiba taarifa zako (taarifa za kifedha, namba za simu, email, nyila/password) n.k. Unaweza kuona unaumiwa jumbe mbalimbali kutoka sehemu usiyoijua au kuona miamala ya kibenki inafanyika pasipo kuifahamu hapo ujue tayari taarifa zako zimeshachukuliwa. tujitahidi kujilinda na kuwa waangalifu pindi tunapotumia simu kwenye mitandao au kupakua/download kitu.
Unaweza pia kusoma makala zetu zingine hapa.
No Comment! Be the first one.