Snapchat mpaka sasa umekua ni mtandao wa kijamii ambao unaangalia huku na kule katika kuhakikisha kuwa inaliteka soko.
Ukiachana na kampuni hiyo kuwa katika michuano mikali na mitandao mingine ya kijamii kama vile Facebook na Instagram bado inazidi kujiboresha
Hapo awali tuliandika kuhusu: Snapchat Yainunua Kampuni Inayotengeneza Bitmoji

Bitmoji ni vikatuni katuni ambavyo mtu anaweza kutengeneza ambavyo kwa namna moja au nyingine vinakuwa vinafanana na mtu. Kwa urahisi ni sawa na kusema vikatuni hivi ni emoji ambazo zinafanana na mtumiaji wa emoji hizo
Tujifunze Jinsi Ya Kutumia Bitmoji Katika Snapchat Sasa!
1. Tengeneza Akaunti Ya Bitmoji
Kama wewe ni mgeni wa Bitmoji, anza kwa kushusha App ya bure ya Bitmoji iOS na Android alafu anza kutengeneza kikatuni. Log In kwa kutumia akaunti yako ya Snapchat na kisha anza kufuata maelekezo.
Utaweza kutengeneza kikatuni cha jinsia ya kiume au ya kike na unaweza ukakimalizia kwa kuweka rangi ya ngozi, nywele, macho na hata muonekano. Ukimaliza hapo hakikisha unaunganisha Bitmoji na Snapchat
2. Kwa Wale Ambao Tayari Wana Akaunti Bitmoji
Kama ulikuwa tayari una akaunti ya Bitmoji cha kufanya ni rahisi sana kwani itakubidi tuu uunganishe akaunti hizo (Bitmoji na Snapchat). Nenda katika settings katika Bitmoji ili kuunganisha akaunti
Jinsi Ya Kutumia Bitmoji Katika Snapchat
Watumiaji wa Snapchat wanaweza wakatuma bitmoji zao na hata emoji zingine wakiwa katika uwanja wa kuchat. Ukiwa katika Snapchat fungua sehemu ya Chat na kisha ingia kwa mtu unaetaka kumtumia bitmoji. Bitmoji utaweza kuipata kupitia kile kialama cha uso
Kama ukitaka Snap zako ziwe na bitmoji ingia sehemu ya kupiga picha au kuchukua video. Piga picha kama kawaida na kisha ingia sehemu ambayo huwa unapata stika, sogea upande wa kulia mpaka utakutana na Bitmoji
Pia watumiaji wanaweza wakatumiana stika za ‘Friendmoji’ wakati wakiwa wana chat na marafiki zao ambao pia wana akaunti za Bitmoji
Jambo hili lisikushangaze kwani hili lote linakuja baada ya Snapchat kuinunua kampuni ya Bitstrip kwa dola milioni 100 za kimarekani mwezi machi.