Kumbuka jukwaa la barua pepe la Gmail ndio jukwaa kubwa kabisa na lenye watumiaji wengi kuliko majukwaa yote.
Pengine sidhani kama kuna mtu mwenye simu janja (Android?) ambae hatumii huduma ya gmail kwa namna moja au nyingine.
Kitu kimoja tulichokizoea ni kwamba kama unakua unatumia huduma hii na ghafla bando lako la intaneti likakata basi utakua huna uwezo kabisa wa kuendelea kutumia huduma hii.
Kwa sasa Google wameonngeza uwezo wa kuweza kutumia Gmail bila hata ya kuwa na mtandao wa intaneti.
Bila ya inteneti utaweza kusoma barua pepe, kujibu barua pepe na kutafuta barua pepe ndani ya mtandao huo
Kizuri ni kwamba Gmail itaweza kufanya mambo haya kwenye maeneo ambayo yana uwezo mdogo wa intaneti au hakuna kabisa.
Ili Kuliwezesha Hili Inabidi Ufuate Njia Hizi!
- Ingia katika mtandao wa Gmail.com cha msingi hapa kujua ni kwamba huduma hii itawezeshwa wakati unatumia kivinjari cha chrome tuu na hakikisha haupo katika “Incognito mode”
- Nenda katika ‘Settings’ na kisha nenda katika ‘See All Settings’
- Ukishafungua hapo nenda katika ukurasa wa ‘Offline’
- Chagua “Enable offline mail”. Ukifanikiwa tuu hilo utaona Gmail itaanza kuonyesha aina mpya ya ‘settings’
- Baada ya hapo utakuwa na uwezo wa kuweza kuchagua machaguo unayotaka kabisa na kisha unaweza chagua “Save Changes”
Mpka hapo utakua tayari umeshaliwezesha hili, sasa endelea kufurahia huduma za Gmail.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, hili umelipokeaje? Je utakuwa unafurahia huduma hii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.