WhatsApp ni mtandao wa kijamii ambao unawezesha watu kuwasiliana kwa ujumbe mfupi, ujumbe wa sauti, kupiga simu pamoja na simu ya video. WhasApp ina watumiaji takribani Bilioni 2 walio hewani kwa mwezi. Ukiwa mjanja unaweza kutumia Whatsapp kukuza biashara yako.
Ili uweze kutumia WhatsApp kukuza biashara zako inabidi upakue app yao ya WhasApp Business ambayo inapatikana Google Playstore itakuwezesha kufanya mambo mbalimbali ikiwemo:
- Kuandika taarifa muhimu kuhusu biashara yako kama; Jina la duka/biashara yako, mahali lilipo, anuani, barua pepe yako, tovuti (kama unayo), maelezo mbalimbali kuhusu huduma unazotoa na nembo yako.
- Kutoa majibu ya Haraka; ukiwa na WhatApp Business utakuwa na uwezo wa kuwajibu wateja wako haraka haraka kutokana na yale maswali ya kujirudia rudia ambayo wateja wengi huwa wanauliza na unaweza kufanya hivi kwa kutunza yale majibu unayowajibu wale wateja wakwanza kuuliza swali hilo.
- Kuwekea alama wateja wako; Unapotumia WhatsApp Business utakuwa na uwezo wa kuwawekea alama watu mbalimbali ulio na namba zao ili kuweza kuwapanga katika mtiririko unaoutaka. Kimfano unaweza kuwawekea alama wateja wako wapya wote ambao umeshachukua oda zao na kuwawekea alama ya tofauti wale wateja ambao umeshamaliza kuwahudumia ili usiwachanganye.
- Kuona Taarifa za ujumbe unaotuma; Ukiwa unatumia Whatsapp Business utakuwa na uwezo wa kuangalia taarifa zako za ujumbe mbalimbali ulizowahi kutuma na kuona kuwa ujumbe upi ulitumwa, ulifika na ulisomwa na mpokeaji.
- Kuonyesha bidhaa ulizonazo au unazo uza; Katika WhatsApp Business utaweza kuonyesha bidhaa zako zote ulizonazo pamoja na taarifa zake kama bei, rangi zilizopo, ukubwa tofauti na jina la bidhaa hiyo. Hakutakuwa tena na usumbufu wa mteja kukuomba umtumie maelezo au picha za bidhaa ulizonazo atakuwa na uwezo wa kuona kila kitu atakachohitaji kujua ili aweze kununua bidhaa kutoka kwako.
No Comment! Be the first one.