Ni wazi kwamba tunaingia katika mtandao wa Netflix kwa kutumia akaunti zetu ambazo pengine tumezilipia sio?
Kwa kupitia akaunti hizo –katika mtandao wa Netflix– kuna uwezekano mkubwa sana tukawa tumeshawahi kuwapa baadhi ya watu na wenyewe wakawa wanazitumia pia.
Kwa namna moja au nyingine inawekana pia ukawa unataka kuwapunguza watu ambao wanatumia akaunti –yako—hiyo na hutaki kuwaambia kwamba watoke.
Kwa mara ya kwanza ili kufanikisha jambo hili ilibidi ubadilishe neno siri (password) la akaunti yako lakini kwa sasa inawezekana kufanikisha hilo bila hata kutumia njia ya kubadilisha neno siri.
Hebu fikiria kama ulishawahi ku’share taarifa za jinsi ya kuingia katika akaunti zako kwa mtu/watu na sasa unawaonea aibu sababu huwezi kuwaambia tuu waache kutumia akaunti yako hivyo inakubidi utumie ujanja ujanja ili kufanikisha kuwatoa.

Kipengele hiki kipya katika mtandao wa Netflix kinafnaya kazi kwa kutambua baadhi ya vifaa ambavyo vinatumiak akatika akaunti yako. Mfano akaunti moja inaweza ikawa inatumiwa na iPhone 14 na vile vile ikawa inatumiwa na Samsung Galaxy Note 10 n.k
Sasa basi ili kufanikisha jambo hilo nenda katika eneo la settings katika akaunti yako ya Netfliz na kisha chagua “Manage Access and Devices,”
Kisha chagua “Sign Out” kwa kile kifaa ambacho unataka akaunti yako isiwe inatumika tena na mpaka hapo utakua umeshafanikisha jambo lako.

Kipengele hichi kinawalazimisha kwa namna moja au nyingine wale ambao hawalipii katika mtandao huo kwa kutumia akaunti yaw engine kalazimika kutumia akaunti zao na kuanza kulipia.
Vile vile hii ni njia moja wapo ya kampuni kujihakikishia kuwa inaziidi kupata mapato mengi kwa sababu akaunti nyingi zitajiunga na kulipia vifurushi tofauti na mwanzo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hili umelipokeaje? Je unadhani ni sahihi kwa mtandao wa Netflix kufanya hivi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.